Habari

SERIKALI KUENDELEZA UJENZI WA MIUNDOMBINU SEKTA ZA MAENDELEO NCHINI

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameeleza nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza ujenzi wa miundombinu imara katika Sekta za maendeleo Nchini.

    Akifungua  Skuli ya Sekondari ya Wanawake ya Ghorofa Tatu ya Utaani iliyojengwa baada kuungua moto Mwezi Machi Mwaka 2022 amesema, Ujenzi wa Skuli hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa baada ya tukio la moto lililoteketeza Skuli ya Awali iliyokuwa na Madarasa 11.

SPIKA WA BUNGE ATOA RAI KUHUSU MABADILIKO YA TABIANCHI

    Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (ipu) Dkt.Tulia Ackson ametoa rai kwa Waandishi wa Habari Nchini kuhakikisha wana ielimisha Jamii kuhusu mabadiliko ya tabianchi kutokana na kuwepo kwa athari zinazotokana na mafuriko.

      Dkt.Tulia ametoa rai hiyo Jijini Dodoma kwenye maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani wakati akizungumza na Waandishi wa Habari,Wadau wa habari wakiwemo Viongozi wa Serikali na Asasi za Kiraia.

SERIKALI KUTOA POSHO LA NAULI NA KUIMARISHA POSHO LA LIKIZO.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshiwa Dr Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha mazingira bora ya Wafanyakazi  kwa kutoa Posho la nauli la kila Mwezi kwa wanaostahiki  pamoja na  kuboresha Posho la  likizo  kwa Wafanyakazi  Nchini

Ameyasema hayo huko Uwanja wa Michezo Gombani katika maadhimisho ya kumbukumbu ya   Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika Kitaifa Kisiwani Pemba

WAFANYAKAZI KUWA NA BIDII NA KUTHAMINI KAZI ZAO

Wafanyakazi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na.kuthamini Kazi zao  ili kufikiya Malengo yao.

Wakitoa Maoni ya Siku ya Wafanyakazi Duniani   baadhi ya Wafanyakazi huko Skuli ya Abdala Sheria  ikiwa ni  katika kuadhimisha siku ya Wafanya kazi Duniani wamesema kuwa    umuhimu wa kuwepo Siku hiyo ni njingi ikiwemo kubadilishana uziwefu na  fursa  ya kujadili pamoja.

Wamesema Mafanikio mengi  yamepatikana pamoja na Maslahi na Mazingira bora kwa Wafanyakazi.

MKOA WA LINDI UMEPOKEA TRILIONI 1.2 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO

Mkoa wa Lindi umepokea Jumla ya Shilingi Tilioni 1.2 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu, Afya, Maji Umeme Barabara na huduma nyingine kwa Kipindi cha Mwezi March 2021 hadi March 2024

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi na Wananchi wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika huko Wilayani Ruangwa 

MOROGORO KUPOTEZA ASILIMIA 10 YA MAENEO YALIYOKUWA MISITUNI

Ukataji Miti na uchomaji ovyo wa Misitu umesababisha Mkoa wa Morogoro kupoteza Asilimia 10 ya maeneo yaliyokuwa misituni huku urejeshwaji wa uoto ukiwa Asilimia 18 ya kiwango kilichofyekwa,wakati kasi ya upotevu wa Misitu ni Asilimi 81.

Maeneo ya uoto karibu Hekta 362,000 hupotea ambapo urejeshaji wake ni Hekta 66,000  hali inaonyesha ni muendelezo wa tabia ya kutumia njia za asili ambazo zinapunguza ubora na upotevu mwingi wa mazao na kuacha Ardhi wazi baada ya kukata Miti.

WATU WENYE ULEMAVU WAHIMIZWA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Simiyu, kimewahimiza Watu wenye Ulemavu na wazee kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura, ili wapate haki ya kuchagua Viongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo wa Simiyu, Shemsa Mohamed, wakati akihutubia Viongozi wanaotokana na Chama hicho Tarafa ya Ngulyati, katika ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa ya kusikiliza Kero za Wananchi na kuzitafutia majawabu.

Amehimiza pia upendo na mshikamano kwa viongozi wa Chama hicho Tawala.

MKURUGENZI SAZANI AWATAKA WANAFUNZI KUYAFANYIA KAZI MAFUNZO YA STADI ZA MAISHA

     Wanafunzi wametakiwa kuyafanyia kazi kwa vitendo Mafunzo ya Stadi za Maisha wanapokuwa katika mazingira ya Skuli na Nje ya Skuli kwa kubuni vitu mbali mbali ambavyo vitawasaidia katika maisha yao ya baadae.

   Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sazani Zanzibar Ndg.Safia Mkubwa Abdallah mara baada ya kutoa Mafunzo ya Stadi za Maisha kwa Wanafunzi, yaliyofanyika huko  Skuli ya Sekondari Fidel Castro Chake Chake Pemba.

UJENZI OFISI ZA MASHEHA KUONGEZA UWAJIBIKAJI

      Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe.Masoud Ali Mohammed, amesema Ujenzi wa Ofisi za Masheha katika Shehia itawawezesha kuongezeka uwajibikaji na Wananchi kuwa huru pindi wanapofata huduma.

   Akitembelea Ujenzi wa Ofisi ya Sheha Shehia ya Ijitimai Mwanakwerekwe, amemtaka Mkandarasi wa Ujenzi huo Kikosi cha KVZ kuharakisha Ujenzi huo ili kuwawezesha Masheha kuongeza ufanisi wa kiutendaji kwa Wakaazi wao.

JENERALI MABEYO AWAVISHA VYEO MAKAMISHNA WAPYA NCAA

    Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu)  amewavisha vyeo maafisa Uhifadhi wakuu waliopandishwa vyeo hivi karibuni katika tukio lililofanyika ofisi za Makao makuu ya NCAA Karatu Mkoani Arusha.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.