Habari

ZURA KUZINGATIA MASLAHI YA NCHI KATIKA UDHIBITI WA NISHATI.

Kamati ya Mawasiliano Ardhi na nishati ya Baraza la Wawakilishi imeihimiza Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Maji na Nishati Zanzibar ZURA kuendelea kuzingatia maslahi ya  Taifa, kwa watoa na wapewa huduma katika kutekeleza Majukumu yao ili Wananchi wapate huduma bora.

BAADHI YA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KUACHA KAULI ZA KIBAGUZI

Umoja wa Vyama vya Siasa Tanzania wamelaani  baadhi ya Wanasiasa kutumia kauli za kuchafua Viongozi pamoja na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  na badala yake wajenge umoja na mshikamano.

 Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusiana na kauli za Makamo Mwenyekiti wa Chadema Tundu LIssu Mwenyekiti wa umoja huo Tanzania Mh  Juma Ali Khatib amesema kuendelea kufanya hivyo ni kuutumia uhuru vibaya na kuwagawa Wananchi.

FEDHA NI NYENZO YA KUENDESHA TAASISI .

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Juma Makungu Juma, amesema Kazi kubwa ya wizara hiyo ni mipango ya kukusanya Fedha na kutumika, kwani hakuna litakalokwenda bila ya Fedha.

Hayo ameyaeleza katika KIkao cha kujitambulisha tokea kuteuliwa kwake kwa Wafanyakazi na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo, Kikao kilichofanyika katika Ukumbi Gombani Mjini Chake Chake.

Amesema bila ya Fedha mipango ya Taasisi hazitaweza kwenda na machoyao wanaitizama Wizara hiyo, ili ziweze kutekeleza Kazi zao.

RAMADHAN BROTHERS KATIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

    Kundi la  'The Ramadhan Brothers' ambao ni washindi wa tuzo za America's Got Talent na ni vijana machachari katika sanaa ya maonyesho ya sarakasi, wamefanikiwa kufika katika kilele kirefu zaidi barani Afrika maarufu kama Paa la Afrika (Uhuru Peak) katika Mlima Kilimanjaro

TANZANIA KINARA WA KULINDA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI AFRIKA MASHARIKI

    Tanzania imeshika nafasi ya kwanza katika nchi zinazolinda Uhuru wa Vyombo vya habari, Afrika Mashariki.

     Nchi hiyo imepanda kutoka nafasi ya 143 kwa mwaka 2023 hadi 97 mwaka huu, kulingana na utafiti uliotolewa na Reporters Without Borders (RSF), Mei 3, 2024.

MAAFISA UTUMISHI WAMETAKIWA KUTOA MAFUNZO KATIKA TAASISI ZAO

    Kuwepo kwa Mafunzo ya Wafanya kazi wa Taasisi za Umma yatachangia uwelewa na kutambua stahiki za Wafanyakazi.

      Akifunguwa Mafunzo kwa Maafisa Utumishi na Maafisa Mafunzo wa Taasisi za Utumishi wa Umma Mkurugenzi Idara ya Mipango ya Rasilimali Watu Ndg.Maulid Shaib Ahmada amesema kuwepo kwa Mafunzo kwa Maafisa hao kutasaidia kufanya kazi kwa bidii katika Sekta zao za kazi.

WANAFUNZI SUZA WATEMBELEA ZBC KUJIFUNZA KWA VITENDO

     Wanafunzi na Walimu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA  Idara ya  Kompyuta na Mawasiliano ya Habari   wamesema Waandishi wa Habari Wachanga Wana Wajibu wa kulinda misingi na ya Habari ili kuimarisha Amani Nchini.

    Wakizungumza katika Ziara ya kujifunza kwa Vitendo huko Shirika la Utangazaji Zanzibar Mnazi Mmoja ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani wamesema hatua hiyo itasaidia shughuli za Maendeleo kufanyika kwa utulivu.

AMANI NA UTULIVU KUONGEZA FURSA ZA KIUCHUMI

      Mamlaka Ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar Zipa imekutana Na Ujumbe Kutoka Chuo Cha Ulinzi Taifa Ndc kwa Zira Ya Kujifunza.

        Akizungumza na Ujumbe Huo Mkurugenzi Mipango Na Utafiti  Alhaj Mtumwa Jecha Amesema, Zipa inajivunia Amani iliopo Nchini kama Ajenda inayoifanya kuitangaza Nchi Duniani kote kupitia fursa zilizopo

KITUO CHA KISASA CHA HUDUMA NA MATIBABU YA SARATANI KIMEZINDULIWA AGA KHAN HOSPITALI

     Naibu Waziri Mkuu ambae pia ni Waziri wa Nishati Dkt.Mashaka Doto Biteko amezindua Kituo cha Kisasa cha huduma na Matibabu ya Saratani katika Hospitali ya Aga-Khan Jijini Dar es salaam.

      Kuzinduliwa kwa Kituo hicho chenye hadhi ya Kimataifa ni Matokeo ya utekelezaji wa mradi mtambuka wa Saratani Tanzania wa Tccp.

TAHADHARI YATOLEWA YA KUTOKEA KIMBUNGA HIDAYA MASHARIKI MWA PWANI YA MTWARA

    Kufuatia utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania juu ya uwezekano wa kutokea kwa Kimbunga Hidaya chenye nguvu ya kati kikiwa umbali wa takribani kilomita 506 kutoka mashariki ya pwani ya Mtwara.

     Aidha, Mamlaka imetabiri mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa baharini inayoonesha uwezekano mkubwa wa kimbunga Hidaya kusogea karibu kabisa na pwani ya Tanzania kuanzia usiku wa  tarehe 2 Mei 2024 na kuendelea hadi tarehe 6 Mei 2024.  

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.