Habari

VIJANA WATAKIWA KUJIWEKEZA KABLA YA KUMALIZA MASOMO

    Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mheshimiwa Salim Alaudin Hasham amewataka Vijana Wanaomaliza Vyuo na wale waliopo Vyuoni kutokukubali kushindwa kwa haraka kuwekeza katika maeneo mbalimbali ili kuwasaidia kutokusubiria ajira kutoka Serikalini au Makampuni Binafsi.

     Mbunge huyo ameyasema hayo Mkoani hapa wakati akizungumza na Wanafunzi hao wa Vyuo mbalimbali kutoka Mkoani Morogoro kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufikiri nje ya box wakati wapo Vyuoni ba baada ya kumaliza Masomo ili kupata mafanikio zaidi.

RAIS DKT.MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA WAPCOS LIMETED YA INDIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na RK Agrawal Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ushauri WAPCOS Ltd kutoka Serikali ya India na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe: 07 Mei 2024.

Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar inahitaji miradi mingi ya uwekezaji katika sekta ya maji na umeme.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameishukuru Serikali ya India kwa kuisaidia Zanzibar katika miradi ya maji.

Naye Mkurugenzi RK Agrawal amesema wako tayari kuendelea kushirikiana na Serikali katika miradi hiyo.

SERIKALI YAJIPANGA KUIMARISHA HUDUMA YA MAJI SAFI KATIKA SKULI ILI KUWAKINGA WANAFUNZI NA MARADHI YA MRIPUKO

     Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina mpango mkakati wa kuimarisha miundombinu ya maji safi na salama katika Skuli ili kuwakinga Wanafunzi na maradhi ya mripuko.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.  Lela Muhammad Mussa amesema kwa kushirikiana na Wadau, watahakikisha mazingira ya kuisoma katika Skuli yanenda pamoja na kuwepo huduma hiyo ya maji safi na salama ili kuimarisha ustawi wa Wanafunzi, Waziri Lela ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano wa Wadau 22 wa Kimataifa hapa Zanzibar.

POLISI YAWASHUKURU WANANCHI WALIOFANYA MABORESHO YA UJENZI WA KITUO CHA POLISI

      Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema litaendelea kuwashukuru wananchi wanaoendelea kushiriki katika jitihada za Serikali katika kuboresha mazingira bora na yakisasa katika vituo vya Polisi Mkoani humo huku likibainisha kuwa litaendelea kutoa huduma bora na za kisasa kwa wananchi

      Hayo yamebainishwa Leo na Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Peter Lusesa wakati akikabidhiwa ofisi ya Upelelezi Wilaya ya Arushabaada ya kufanyiwa marekebisho na wadau wa masuala ya usalama ili kutoa huduma bora kwa wateja.

ZAIDI YA BILLIONI 11 ZATUMIKA KAMA KIFUTA JASHO WAATHIRIKA WA WANYAMA WAKALI

      Serikali imelipa kiasi cha shilingi bilioni 11,085,850,400 kama kifuta jasho na kifuta machozi kuanzia Mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Machi, 2024, kwa wananchi waliothirika na changamoto ya wanyama wakali na waharibifu.

MADKTARI BINGWA NA WABOBEZI WAPIGA KAMBI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA LINDI

     Madaktari Bingwa na Wabobezi wa Rais samia zaidi ya 50 wameweka kambi maalumu ya matibabu ya Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi kwa siku 5 kuanzia Mei 6 hadi 10.

      Akizindua utoaji wa  matibabu hayo mkuu wa wilaya ya Lindi, Ndg. Shaibu Ndemanga kwa  niaba ya mkuu wa mkoa wa Lindi mkuu huo  amesema huduma hizo za kibingwa zitarahisisha  kwa kiasi kikubwa huduma kuwafikia wananchi na hivyo kupunguza gharama ya  kusafiri kwenda nje ya mkoa huo kufuata huduma hizo

WAHITIMU MAFUNZO YA AWALI YA KIJESHI WATAKIWA KUWA WAZALENDO

     Brigedia Jenerali, Charles Peter Feluzi amewataka vijana waliohitmimu  mafunzo ya awali ya kijeshi ya jeshi la kujenga Taifa (JKT)  kuwa wazalendo waaminifu na waalibifu katika kusimamia na kuijenga  nchi yao

     Brigedia Jenerali Charles Feluzi ametoa rai hiyo wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa kujitolea oparesheni ya miaka 60 ya jeshi la kujenga Taifa JKT kikosi 843 huko Nachingwea

WAAJIRI NCHINI KUWAHAMASISHA WATUMISHI KUJAZA MFUMO PEPMIS

Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ Mhandisi Zena Said amewaelekeza waajiri wote Nchini kupitia Mtandao wa mameneja rasilimali Watu Barani Afrika Tawi la Tanzania kuendelea kuwahamasisha Watumishi kujaza Mfumo Pepmis kama Takwa la Kisheria. 

SHILINGI TRILIONI 2.72 KUIMARISHA MAWASILIANO YA SIMU

Kuimarika kwa Mawasiliano katika Ziwa Victoria, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeandaa hati ya makubaliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) pamoja na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwa ajili ya Ujenzi wa Minara Mitatu ya Mawasiliano ya Simu. 

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 ambapo ameliomba Bunge kuidhinishiwa ujumla ya  Trilioni 2.72.

WEMA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA VYUO VIKUU VYA CHINA

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema ujio wa Wageni kutoka Chuo cha Hunan  Nchini China kutaendeleza Ushirikiano wa Kielimu  Zanzibar

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh Leila Muhammed Mussa amesema hayo Ofisini  kwake Mazizini wakati alipokuwa akizungumza na Wageni kutoka Chuo Kikuu cha Khunan Nchini China.

Amesema mambo mbali mbali wamekubaliana nao ikiwa ni pamoja kueka ushirikiano Mzuri katika mazingira ya Elimu kwa Wanafunzi wa Maandalizi, Secondari na Chuo Vikuu mbali mbali vilivyopo  Nchini

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.