Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema ujio wa Wageni kutoka Chuo cha Hunan Nchini China kutaendeleza Ushirikiano wa Kielimu Zanzibar
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh Leila Muhammed Mussa amesema hayo Ofisini kwake Mazizini wakati alipokuwa akizungumza na Wageni kutoka Chuo Kikuu cha Khunan Nchini China.
Amesema mambo mbali mbali wamekubaliana nao ikiwa ni pamoja kueka ushirikiano Mzuri katika mazingira ya Elimu kwa Wanafunzi wa Maandalizi, Secondari na Chuo Vikuu mbali mbali vilivyopo Nchini
Makamo wa Raisi kutoka Chuo Kikuu cha Hunai kutoka Nchini China Wangu Weibin amesema lengo la ni kujenga Ushirikiano na Vyuo Vikuu na sehemu nyengine ambapo hadi sasa tayari ya washaungana na Vyuo Vikuu zaidi ya Mia Moja.
stories
standard