Habari

MKANDARASI AMETAKIWA KUMALIZA KIWANJA CHA KUFURAHISHIA WATOTO PAJE.

waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohammed ametoa Mwezi Mmoja kwa Mkandarasi wa Ujenzi wa Kituo cha kufurahishia Watoto Paje, kukamilisha Ujenzi huo.

Akikagua Ujenzi huo ulioanza Mwezi Febuari Mwaka jana, amesema hajaridhishwa na hatua ya Ujenzi huo ambao umechukua muda haujakamilika na kuwakosesha Walengwa ambao ni Watoto fursa ya kulitumia eneo hilo.

MAJESTIC CINEMA KUFANYIWA MATENGENEZO

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Kimataifa (UNESCO) linatarajia kulifanyia matengenezo Jengo la Majestic Cinema la Mji Mkongwe na kuwa Kituo Kikuu cha Utamaduni.

Akizungumza katika Warsha yenye lengo la kujadili mikakati ya kulitengeneza jengo hilo kati ya Wataalamu wa Unesco na Watendaji wa Serikali ya Zanzibar Waziri wa elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Lela Mohamed Mussa amesema hatua hiyo itaongeza fursa kwa Zanzibar kuimarisha sekta ya Utalii kutokana na kuutunza Mji Mkongwe na kuongeza hadhi ya Vivutio vyake. 

MASHEHA WAMETAKIWA KUORODHESHWA WAZEE WALIOFIKIA MIAKA 70 KATIKA PENCHENI JAMII

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe amewasisitza Masheha Mkoa wa Kusini Unguja kuwaorodhesha Wazee wote ambao wameshafikia umri wa kupokea Pencheni Jamii ili waweze kunufaika na fursa na haki hiyo.

Akizungumza na Masheha hao amesema ni vyema kwa Masheha kuangalia Wazee ambao wana mkanganyiko wa vielelezo vya Vitambulisho kutumia njia mbadala kuhakikisha hawakosi haki yao hiyo kwa kisingizio chochote.

WATUMISHI WA ZHSF WAMETAKIWA KUENGEZA KASI ZA USAJILI WA WANACHAMA.

Watumishi wa Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar ZHSF wametakiwa kuengeza kasi za usajili wa Wanachama ambazo wanaweza kuwasaidia kupata huduma za Matibabu kwa Urahisi wakati wa matumizi ya Mfuko wa huduma ya Afya ili kuona lengo la huduma kwa wote linafikiwa 

BARABARA YA KUSINI KUANZA KUTUMIKA KESHO ASEMA WAZIRI BASHUNGWA

     Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amaendelea kusisitiza ifikapo kesho Alhamisi Mei 9,2024 mawasiliano ya barabara barabara ya Lindi - Dar es Salaam yatarejea ambapo tayari eneo la somanga limeanza kupitika .

      Bashungwa ameyasema hayo Mei 08, 2024 Mkoani Lindi wakati akisimamia zoezi la urejeshaji wa miundombinu ya barabara hiyo ambayo iliharibiwa mvua za El-Nino  siku  ya Jumamosi zilizombatana na Kimbunga Hidaya.

RAIS DK.MWINYI APOKEA SALAMU ZA POLE KUTOKA KWA MAMA ANNA MKAPA

       Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea  salamu za pole ya kifo  cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mzee Ali Hassan Mwinyi kutoka kwa Mjane wa  Rais Mstaafu Marehemu Benjamin  William Mkapa, Mama Anna Mkapa aliyefika Ikulu Migombani tarehe 08 Mei 2024.

      Mama Anna Mkapa ambae wakati wa Msiba wa Mzee Mwinyi alikua nje ya nchi amemuombea kwa Mwenyezi Mungu Marehemu Mzee Mwinyi Mola ampokee hali ya kuwa amemridhia.

ZURA YATOA TAARIFA YA KUPANDA KWA BEI YA PETROLI NA KUSHUKA KWA BEI YA DIZELI

    Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetoa taarifa ya Bei za mafuta kwa Mwezi Mei 2024 zitakazoanza kutumika Alhamisi 09/05/204.

     Hii ni kutokana na Wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya Bei za mafuta duniani, pamoja na Kupanda au kushuka kwa thamani ya fedha za kigeni zinazotumika kununulia mafuta.

MAKONDA YUPO TAYARI KUPOTEZA KILA KITU ILI KUSIMAMIA HAKI MKOANI ARUSHA

     Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Christian Makonda amewaambia wakazi wa Mkoani Arusha kuwa yupo tayari kupoteza chochote alichonacho ili walau Mwananchi mmoja wa Arusha aweze kupata haki yake na kunufaika na cheo chake.

      Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye Kliniki ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi amesema hawezi kukaa kwenye kiti cha Mkuu wa Mkoa ilihali wananchi anaowaongoza wakiteseka na changamoto mbalimbali ambazo zipo ndani ya Mamlaka yake ya Kiuongozi.

WEZI WA PIKIPIKI KATIKA MASHEREHE, MISIBA NA SEHEMU ZA IBADA WATIWA MBARONI NAJESHI LA POLISI

       Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za wizi wa pikipiki katika maeneo ya mikusanyiko ya watu ikiwemo kwenye harusi, misiba na nyumba za ibada.

RAIS DKT.SAMIA ASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na viongozi mbalimbali wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.