Watumishi wa Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar ZHSF wametakiwa kuengeza kasi za usajili wa Wanachama ambazo wanaweza kuwasaidia kupata huduma za Matibabu kwa Urahisi wakati wa matumizi ya Mfuko wa huduma ya Afya ili kuona lengo la huduma kwa wote linafikiwa
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamiss Hafidh ameyasema hayo katika uzinduzi wa Mashirikiano baina ya Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar ZHSF na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF amesema mashirikiano hayo yataenda kutoa matokeo ya huduma bora kwa Wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania ambalo ndio lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huo
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar Yassin Ameir Juma na Mkurugenzi Mkuu NHIF wamesema Mashirikiano hayo yataweza kuleta matokeo mazuri ambao utaweza kuwafanya kwa pamoja kwa kutoa huduma zaidi ambayo wananchi wanatakiwa kuzipata kutoka kwenye mifuko ya huduma hizo
Mwenyekiti wa Bodi ya ZHSF Mbarouk Omar Mohmed na Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Juma Muhimbili wamesema mashirikiano haya yanonesha taswira ya upatikanaji wa huduma muhimu za Afya kwa Wazanzibari na Watanznia kwa ujumla
Nassor Salum Muwakilishi wa Chama cha Waajiri Sekta Binafsi na Mwajum Hamiss Othmn Muwakilishi wa Vyama vya Wafanyakazi
Wamesema uharaka wa kuanza kufnyakazi kwa makubaliano hayo unahitajika ili kuona mabdiliko ambayo yanaenda kutokea kutokana na Mfuko huu wa huduma za Afya na kuondoa matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo Wananchi wanapotaka huduma mbalimbali katika Vituo vya Afya