MAJESTIC CINEMA KUFANYIWA MATENGENEZO

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Kimataifa (UNESCO) linatarajia kulifanyia matengenezo Jengo la Majestic Cinema la Mji Mkongwe na kuwa Kituo Kikuu cha Utamaduni.

Akizungumza katika Warsha yenye lengo la kujadili mikakati ya kulitengeneza jengo hilo kati ya Wataalamu wa Unesco na Watendaji wa Serikali ya Zanzibar Waziri wa elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Lela Mohamed Mussa amesema hatua hiyo itaongeza fursa kwa Zanzibar kuimarisha sekta ya Utalii kutokana na kuutunza Mji Mkongwe na kuongeza hadhi ya Vivutio vyake. 

Mwakilishi wa UNESCO Nchini Tanzania Michael Toto amesema UNESCO itaendelea kuiunga Mkono Serikali ya Zanzibar katika kuyafikia malengo yake ya kuuhifadhi Mji huo ili kuleta manufaa zaidi kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Balozi wa Japan na Balozi wa Saudia Arabia Nchini Tanzania wamesema kupitia UNESCO watafanikisha utekelezaji wa Mradi wa kulifanyia matengenezo Jengo la Majestic Cinema lenye historia ya muda mrefu Zanzibar.

Jengo la Majestic Cinema awali  lilijengwa mnamo mwaka 1921 ambapo Watu kutoka mataifa mbalimbali walikutana kuangalia Filamu na kubadilishana uzoefu na baadae kujengwa tena baada ya kuungua moto mnamo Mwaka 1951.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.