MKANDARASI AMETAKIWA KUMALIZA KIWANJA CHA KUFURAHISHIA WATOTO PAJE.

MHE. MASSOUD ALI MOHAMMED

waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohammed ametoa Mwezi Mmoja kwa Mkandarasi wa Ujenzi wa Kituo cha kufurahishia Watoto Paje, kukamilisha Ujenzi huo.

Akikagua Ujenzi huo ulioanza Mwezi Febuari Mwaka jana, amesema hajaridhishwa na hatua ya Ujenzi huo ambao umechukua muda haujakamilika na kuwakosesha Walengwa ambao ni Watoto fursa ya kulitumia eneo hilo.

Aidha Waziri Masoud ameagiza kuwa Ujenzi wa Kiwanja hicho ambao utaepusha kwa Watoto kufata huduma hiyo masafa ya mbali, uwe wa Kiwango cha ubora kwa kuzingatia usalama wa Watumiaji.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema Ofisi yake itasimamia ili kuhakikisha Ujenzi huo unakamilishwa kama ilivyoagizwa.

Nae Kaimu  Mkurugenzi Halmashauri ya Kusini Unguja, Juma Mohammed Chande, amesema maelekezo yaliyotolewa yamelenga kujenga hisia za Kimaendeleo kwa utekelezaji wa Miradi iliyoanzishwa.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.