MADKTARI BINGWA NA WABOBEZI WAPIGA KAMBI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA LINDI

Madaktari Bingwa

     Madaktari Bingwa na Wabobezi wa Rais samia zaidi ya 50 wameweka kambi maalumu ya matibabu ya Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi kwa siku 5 kuanzia Mei 6 hadi 10.

      Akizindua utoaji wa  matibabu hayo mkuu wa wilaya ya Lindi, Ndg. Shaibu Ndemanga kwa  niaba ya mkuu wa mkoa wa Lindi mkuu huo  amesema huduma hizo za kibingwa zitarahisisha  kwa kiasi kikubwa huduma kuwafikia wananchi na hivyo kupunguza gharama ya  kusafiri kwenda nje ya mkoa huo kufuata huduma hizo

     Tunatoa shukrani za dhati kwa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya utoaji wa Huduma za Afya kwa kuhakikisha anapeleka fedha za ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya pamoja na manunuzi ya vifaa tiba” amesema Ndemanga

     Aidha, Ndemanga amewaomba wananchi wote wenye matatizo ya kiafya kuhudhuria katika kambi hiyo ili kuonana na kutibiwa na Madaktari Bingwa na Bingwa bobezi ambapo itasaidia kuwapunguzia gharama za kusafiri umbali mrefu nje ya mkoa kufuata Huduma Hizo

       Dkt.Alexander Makalla mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Sokoine amesema ili kuwafikia wananchi wengi zaidi huduma za kumuona daktari zitatolewa bure isipokiwa kwa wagongwa waliokuwa na Bima za Afya huku mgonjwa akitakiwa asilimia 70 kwa huduma za vipimo, upasuaji na dawa

     Amesema huduma zitakazotolewa ni pamoja na Magonjwa ya wanawake na uzazi, Magonjwa ya Watoto, Magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya ngozi, Magonjwa ya kinywa na meno.

     Huduma zingine ni Magonjwa ya macho, Magonjwa ya Afya ya akili pamoja na magonjwa ya pua, koo na Masikio pia huduma za mazoezi Tiba na viungo, upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi na matiti pamoja na huduma za vipimo vya maabara, mionzi na upasuaji

     Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya, Irene Katarahiya akatumia fursa hiyo kuwahasa wananchi kujiunga na mfuko huo ili waweze kunufaika na huduma lukuki

     "Kwa Mkoa wa Lindi hii ni fursa hasa kwa wale wenye kadi ya mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  kwa sababu kadi yake inamuwezesha kumuona daktari yeyote katimu hii ambayo tuna Madaktari zaidi ya hamsini hapa Mkoani Lindi hivyo nitumie fursa hii kuwahasa wananchi amabo bado hawajakata kadi za Bima za Afya kufanya hivyo ili kuweza kunufaika na fursa zijazo".

    Nao baadhi ya wananchi waliofika kupata matibabu hayo wakamshukuru rais samia kwa kuwasogezea huma hizo karibu yao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.