VIJANA WATAKIWA KUJIWEKEZA KABLA YA KUMALIZA MASOMO

Mbunge  Morogoro

    Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mheshimiwa Salim Alaudin Hasham amewataka Vijana Wanaomaliza Vyuo na wale waliopo Vyuoni kutokukubali kushindwa kwa haraka kuwekeza katika maeneo mbalimbali ili kuwasaidia kutokusubiria ajira kutoka Serikalini au Makampuni Binafsi.

     Mbunge huyo ameyasema hayo Mkoani hapa wakati akizungumza na Wanafunzi hao wa Vyuo mbalimbali kutoka Mkoani Morogoro kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufikiri nje ya box wakati wapo Vyuoni ba baada ya kumaliza Masomo ili kupata mafanikio zaidi.

     Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabir Makame amewahimiza Vijana hao kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kutengeneza mahusiano na watu mbalimbali ili kutengeneza msingi mzuri wa kuweza kufanikiwa kwenye shughuli zao.

     Baadhi ya Wanafunzi wa Vyuo wamesema Vijana wanashindwa kuendeleza malengo yao kutokana na kukosa Mitaji pamoja na Elimu ya usimamizi wa mitaji.

Image removed.Image removed.Image removed.Image removed.Image removed.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.