WAHITIMU MAFUNZO YA AWALI YA KIJESHI WATAKIWA KUWA WAZALENDO

Wahitimu jkt

     Brigedia Jenerali, Charles Peter Feluzi amewataka vijana waliohitmimu  mafunzo ya awali ya kijeshi ya jeshi la kujenga Taifa (JKT)  kuwa wazalendo waaminifu na waalibifu katika kusimamia na kuijenga  nchi yao

     Brigedia Jenerali Charles Feluzi ametoa rai hiyo wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa kujitolea oparesheni ya miaka 60 ya jeshi la kujenga Taifa JKT kikosi 843 huko Nachingwea

     Amewataka wahitimu hao kutumia Mafunzo waliyoyapata katika kuijenga na kuilinda Nchi  kwa kuzingatia kiapo chao.

     Pia amewataka kujiepusha na matumizi yasiyofaa katika mitandao ya kijamii badala yake waitumie mitandao katika kujifunza na kwa manufaa bila kuvunja sheria na Taratibu za Nchi yao.

      Luteni Kanali Nyagalu  Malecela ni mkuu wa kikosi cha 843 Nachingwea amesema vijana hao wakiwa kambini hapo kwa majuma 16  wameweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya awali ya kijeshi na kuwajenga vijana hao kuwa wakakamavu pamoja na wazalendo

     Awali akitoa salamu za Wilaya katibu tawala wa wilaya ya Nachingwea Haji Mabruck Balozi aliwasihi wahitimu kuendelea kujiendeleza kimasomo.

     “Kupitia Elimu kijana unaweza kuwa Meneja wa Benki, Mkuu wa kikosi, Mbunge, Waziri na Hata Rais hivyo niwasihi vijana kujiendeleza kimasomo ili mfikie malengo yenu" alisema Balozi.

     Nao baadhi ya wahitimu  wakaeleza umuhimu wa mafunzo hayo sambamba na kuwasihi vijana wengine kujiunga na jeshi hilo

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.