Kamati ya Mawasiliano Ardhi na nishati ya Baraza la Wawakilishi imeihimiza Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Maji na Nishati Zanzibar ZURA kuendelea kuzingatia maslahi ya Taifa, kwa watoa na wapewa huduma katika kutekeleza Majukumu yao ili Wananchi wapate huduma bora.
Wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe Yahya Rashid Abdallah akizungumza katika Ofisi za Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji EWURA na Watendaji wa Zura katika ziara ya kujifunza na kuiongezea uwezo Mamalaka hiyo katika kutekeleza majukumu yake.
wameitaka Mamlaka hiyo kuwajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu kwa na kuhakikisha kuwa wanatoa huduma zenye tija na ushindani pamoja na ufanisi wa Kiuchumi utakaochochea upatikanaji wa huduma za Maji, Umeme, Mafuta na Gesi ili kuyafikia makundi yote Mjini na Vijijini.
Viongozi wa ZURA na EWURA wameihakikishia kamati hiyo kuwa mamlaka hizo zimeendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwa na lengo la kuhakikisha huduma za Maji na Nishati zinapatikana kwa uhakika na gharama nafuu kwa Wananchi.
Kamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi ipo Jijini Dodoma katika Kazi zake kawaida na kujifunza mambo mbali mbali.