Tanzania imeshika nafasi ya kwanza katika nchi zinazolinda Uhuru wa Vyombo vya habari, Afrika Mashariki.
Nchi hiyo imepanda kutoka nafasi ya 143 kwa mwaka 2023 hadi 97 mwaka huu, kulingana na utafiti uliotolewa na Reporters Without Borders (RSF), Mei 3, 2024.
Kenya iko katika nafasi ya pili ikipanda kutoka 116 hadi 102 wakati Somalia inashika mkia ikiwa ni ya 141 duniani.
Utafiti huo umeangazia mambo mbalimbali yakiwemo misingi ya kisheria, hali ya kiuchumi, hali ya kisiasa, usalama wa wanahabari na dhana ya kijamii na kitamaduni.
stories
standard