Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshiwa Dr Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha mazingira bora ya Wafanyakazi kwa kutoa Posho la nauli la kila Mwezi kwa wanaostahiki pamoja na kuboresha Posho la likizo kwa Wafanyakazi Nchini
Ameyasema hayo huko Uwanja wa Michezo Gombani katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika Kitaifa Kisiwani Pemba
Mheshimiwa Rais amesema ili kupatikana kwa ufanisi unaotokana na azma ya utekelezaji huo ni wajibu kwa Wafanyakazi kutekeleza majukumu yao kwa bidii umoja na uwajibikaji katika sehemu zao za kazi
Aidha aimetaka Wizara ya kazi kukaa pamoja na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) kila robo ya Mwaka ili kuzungumza na kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya Wafanyakazi pamoja na kuangalia namna bora ya kuwaletea wafanyakazi maslahi na haki stahiki
Akisoma risala ya Wafanyakazi katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) Khamis Mwinyi Moh'd amesema Waajiri na Waajiriwa watakuwa na kazi kubwa katika kufikia uwajibikaji makazini iwapo hakutakuwepo majadiliano ya pande zote za Kiutendaji.
Naye Waziri wa kazi uchumi na uwekezaji Zanzibar Mheshimiwa Sharif Ali Sharif amesema Wizara itahakikisha inasimamia vyema haki na wajibu wa Waajiri na Waajiriwa ili kuondosha lawama na malalamiko ambayo yanazorotesha kasi ya utendaji kazi
Kaulimbiu ya Mei Mosi Mwaka huu ni kuimarika kwa maslahi na mazingira ya kazi ni msingi wa ufanisi kazini