MOROGORO KUPOTEZA ASILIMIA 10 YA MAENEO YALIYOKUWA MISITUNI

MKUU WA MKOA WA MOROGORO

Ukataji Miti na uchomaji ovyo wa Misitu umesababisha Mkoa wa Morogoro kupoteza Asilimia 10 ya maeneo yaliyokuwa misituni huku urejeshwaji wa uoto ukiwa Asilimia 18 ya kiwango kilichofyekwa,wakati kasi ya upotevu wa Misitu ni Asilimi 81.

Maeneo ya uoto karibu Hekta 362,000 hupotea ambapo urejeshaji wake ni Hekta 66,000  hali inaonyesha ni muendelezo wa tabia ya kutumia njia za asili ambazo zinapunguza ubora na upotevu mwingi wa mazao na kuacha Ardhi wazi baada ya kukata Miti.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Mradi wa uwezeshaji Jamii katika usimamizi endelevu wa Misitu na Nishati mbadala(USEMINI),Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh.Adamu Malima amesema udhibiti wa kuokoa Misitu ni kuhakikisha Wananchi wanapanda Miche Milioni moja  ya Mazao mbadala kwaajili ya kurudisha uoto  wa Miti katika maeneo yaliyoharibiwa kwa kuchoma Mkaa.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Helvetas hasa maeneo ya Vijiji unaonyesha  kuna zaidi ya Kaya 740 lakini asilimia Mbili  ndio wanatumia Nishati Mbadala,sababu ikiwa ni ukosefu wa Elimu 

Mkaa Mbadala  ambao kwa sasa Bei yake ni Sh.450-550 kwa Kilo ambayo ipo chini kuliko wa kawaida unaouzwa kwa bei ya sh.600-800 kwa Kilo,ambapo Mkaa mbadala hupunguza gharama ya Nishati ya kupikia kwa Mwaka angalau Asilimia 25 sawa na Sh.216,000.

Mradi wa usemini unatekelezwa na Jamii ikiwemo Wanawake na Wanaume katika Halmashauri Nne za Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na wadau kwenye Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kupitia Mnyororo wa Thamani wa Nishati Mbadala endelevu na ufanisi wa usambazaji wa Nishati Mbadala,Kuvumbua fursa,kuongeza kipato na kupunguza uharibifu wa Misitu ili kudhibiti Madhara ya mabadiliko ya Tabianchi.

Mradi wa usemini utatekelezwa kwa muda wa Miaka 3 ukiwa unaofadhiliwa na umoja wa Ulaya kwa Asilimia 90 na Shirika la Helvetas Asilimia 10 wenye Jumla ya bajeti ya euro Milioni 2,222,222

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.