SERIKALI KUJENGA MIUNDO MBINU WEZESHI YA ELIMU

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Ujenzi wa Mindombinu ya Elimu Nchini unalengo la kuimarisha sekta ya Elimu iliyoko kwenye mageuzi makubwa ya maendeleo.

Akifungua Skuli ya Sekondari Hassan Khamis Hafidhi iliopo Mtopepo, ikiwa ni mwendelezo wa shamrashamra za maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, amesema, nia ya serikali ni kupunguza wengi wa Wanafunzi Madarasani na kubakisha wastani wa Wanafunzi 45 kwa kila Darasa, pamoja na kuweka Mkondo mmoja kwa Skuli zote za unguja na Pemba.

Akizungumzia mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana kwenye sekta ya Elimu, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa sekta hiyo imevuka malengo ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi ccm 2021/ 2025 kwa kuimarisha Miundombinu ya kisasa, ikiwemo Makataba, Madarasa, Maabara na Madawati, pamoja na kuzingatiwa Maslahi ya Walimu na kuongeza ajira za Walimu wa hesababati na Sayansi, Unguja na Pemba.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe Lela Muhamed Mussa, ameahidi kuisimamia kwa ufanisi Miradi yote inayotekelewa na kusimamiwa na Wizara hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khamis Abdalla amesema ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Hassan Khamis Hafidh wa Ghorofa Tatu umenza Mwezi Februari Mwaka 2022 hadi uliposita Mwezi wa Nane Mwaka huo na baadae kukabidhiwa Chuo cha mafunzo kwa ajili ya kuuendeleza hadi kukamilika kwake.

Akizungumza kwa Niaba ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Magharibi Kichama, Muhamed Rajab Sudi ameusifu juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Uongozi wa Dk. Mwinyi katika kuleta maendeleo Nchini.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.