Watu 13 Wamefariki Dunia na wengine 6 Wamejeruhiwa vibaya baada ya Basi dogo la Abiria aina ya Hiace kugongana uso kwa uso na Roli la Mafuta kwenye eneo la Somanga Wilaya kilwa Mkoa wa Lindi.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa Mbili Asubuhi na kuhusisha Basi dogo la Abiria aina ya Hiace lenye namba za usajili t 707 DSX lililokuwa likitokea Somanga kuelekea Kilwa Kivinje na Roli la Mafuta lenye Namba za usajili t 224 dzt lenye Tela namba t 920 CUK lililokuwa likitokea Mtwara kuelekea Dar Es Salaam.
Akithibitisha Ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa lindi ACP John Imori amesema Madereva wa Magari yote Mawili wanashikiliwa na Jeshi hilo kwa Uchunguzi.
Akitoa Kauli ya Serikali kuhusu Mazishi ya Miili ya Marehemu na Matibabu kwa Majeruhi wa Ajali hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Zuwena Omary amesema taratibu za kukabidhi Miili ya Marehemu waliopata Ajali zinachukuliwa.