Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu Mh.Ali Suleiman Ameir Mrembo, amesema Takwimu za idadi ya watu hapa Nchini ni nyenzo muhimu ya kupanga, kutekeleza na kufatilia sera na mipango ya maendeleo.
Akifungua Kongamano la Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, katika Ukumbi wa Chuo cha Polisi Ziwani, amesema Takwimu za Idadi ya Watu zinawezesha kupatikana uwelewa juu ya muundo wa Jamii na Maeneo ya Makaazi, ili kuweza kufanya maamuzi sahihi yanayolenga mahitaji halisi ya Wananchi.
Akizumgumzia kuhusu Muungano wa Tanzania amewataka Vijana wa Vyuo Vikuu kuchukua jukumu la kuwaelimisha Vijana wenzao umuhimu wa uwepo Muungano na kuwataka kuwa Wazalendo kwa kushiriki kwenye masuala ya maendeleo ya taifa lao.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar Salum Kassim Ali na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makaazi ya Mwaka 2022 Balozi Mohammed Haji Hamza wamesema Muungano wa Tanzania, unahitaji kurithishwa kwa Vizazi vijavyo kwa umeimarisha Umoja wa Wananchi wake.
Nae Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Dk.Islam Seif Salim amesema kuna umuhimu kwa Kizazi cha sasa kupewa Taaluma sahihi ya uwepo wa Muungano, kwaniumekuwa ukipotoswa kwa makusudi .
Kongamano lilihusisha mjadala unaozungumzia Muungano, ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni idadi ya Watu na Maendeleo ndani ya Muungano.