AKAUNTI YA NMB PESA ISIYO NA MAKATO YAZINDULIWA KANDA YA KUSINI

NMb Account

    Benki ya NMB kanda ya kusini imezindua kampeni   ya kuhamasisha na kuwawezesha watu wengi kufungua akaunti ili waweze kunufaika na faida za kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa fedha.

    Kampeni hiyo inayoitwa “NMB Pesa Haachwi Mtu” kwa kanda ya kusini imezinduliwa rasmi Mkoani Lindi katika viwanja vya shule ya Msingi Mnolela halmashauri ya Mtama kwa kufanya bonanza la michezo mbalimbali.

    Michezo hiyo ni pamoja na mpira wa miguu,  kukimbia na magunia , kukuna nazi , kunywa soda , mpira wa pete pamoja na mazoezi ya viungo. 

    Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja wa NMB kanda ya kusini Faraja Ng'ingo  alisema lengo kuu la kampeni hiyo kupitia huduma ya NMB Pesa Akaunti ni kusaidia kuongeza idadi ya watu wenye akaunti za benki nchini na wale wanaohudumiwa na taasisi hiyo ambao sasa hivi ni zaidi ya milioni sita.

    Alisema NMB kama benki kinara nchini inawajibu wa kusaidia kutatua changamoto hiyo ndiyo maana ukafanyika uamuzi wa kuendesha kampeni hiyo inayowalenga hasa wananchi wa kawaida hususani mama ntilie, wamachinga , waendesha boda boda na hata wakulima .

     Hata hivyo  Meneja Ngingo alibainisha kuwa   akaunti ya NMB Pesa inafunguliwa kwa TZS 1,000 tu na aina makato ya kila mwezi ambapo  lengo la unafuu huo ni kuondoa ile dhana ya kuwa kufungua akaunti ni jambo aghali linalohitaji fedha nyingi.

    “Ufunguaji NMB Pesa Akaunti utafanyika kirahisi sana mahala popote kidijitali na maafisa mauzo wetu ambao ni maalumu kwa ajili ya kazi hiyo,”  alisema Meneja Ng'ingo 

    “Kupitia mchakato huu, tunataka kutimiza ndoto za wale wote wanaohitaji kuwa na akaunti za benki huku akibainisha  kuwa NMB Pesa Akaunti ina faidi lukuki.

    Alizitaja miongoni mwa Faida hizo ni pamoja na kuunganishwa na huduma ya NMB Mkononi ambayo faida zake nyingi ni pamoja na mikopo ya Mshiko Fasta isiyokuwa na dhamana inayoaanzia TZS 1,000 hadi TZS 500,000.

      Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi Udhaifa Rashid alitumia nafasi  hiyo kuwahasa wananchi kuitumia fursa ya NMB Pesa Akaunti kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.