JUMUIYA YA VIJANA NI TEGEMEO KATIKA CHAMA CHA MAPINDUZI

Mwenyekiti wa CCM

     Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana UVCCM Jokate Mwegelo, amesema Jumuiya hiyo ni tegemeo katika Chama cha Mapinduzi hivyo atahakikisha inachangia kuleta ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

     Akizungumza na Vijana wa Chama cha Mapinduzi baada ya Mapokezi  yake ikiwa ni Ziara ya kwanza tokea ashike tena wadhifa huo,  Jokate amesema Vijana wana kazi wa kuimarisha Chama hivyo Serikali kwa kuthamini kundi hilo itaendelea kubuni mbinu za kuwawezesha kuzifikia fursa za kiuchumi.

    Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Mkoa  wa Mjini Hussein Ayoub Ame amewahakikisha Vijana kuwa Serikali itaendeleza mipango ya kiuchumi ili kuondokana na tatizo la ajira.

    Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama Talib Ali Talib amesema  wanataka mabadiliko katika Mwaka 2025 katika kukisimamisha Chama kwa kupata ushindi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.