SERIKALI KUTOA POSHO LA NAULI NA KUIMARISHA POSHO LA LIKIZO.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshiwa Dr Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha mazingira bora ya Wafanyakazi  kwa kutoa Posho la nauli la kila Mwezi kwa wanaostahiki  pamoja na  kuboresha Posho la  likizo  kwa Wafanyakazi  Nchini

Ameyasema hayo huko Uwanja wa Michezo Gombani katika maadhimisho ya kumbukumbu ya   Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika Kitaifa Kisiwani Pemba

SERIKALI KUJENGA MIUNDO MBINU WEZESHI YA ELIMU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Ujenzi wa Mindombinu ya Elimu Nchini unalengo la kuimarisha sekta ya Elimu iliyoko kwenye mageuzi makubwa ya maendeleo.

MAFUNZO KWA KAMATI ZA SADCOPAC YATASAIDIA KUFANIKISHA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kufanyika kwa Mkutano wa kutoa Mafunzo ya kuzijengea uwezo Kamati za kuchunguza hesabu za Serikali za Mabunge ya Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCOPAC) kutasaidia kuchochea kasi ya maendeleo kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

WAISLAM KUENDELEZA MEMA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al haj Dkt Huseein Mwinyi amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kuendeleza mema waliyodumu nayo katika kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuimarisha ustawi wa Jamii.

Akizungumza katika hafla ya Baraza la Eid huko Ziwani amesema kufanya hivyo kutaweza kuidumisha Nchi katika hali ya Amani na Usalama.

SERA YA UCHUMI WA BULUU KURAHISISHA MAENDELEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Sera ya Uchumi wa Buluu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina Dhamira ya kuimarisha uchumi wa Nchi kwa haraka. 

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege Mkoa wa Mjini Magharibi alipozindua duru ya kwanza ya utoaji wa Vitalu kwa Kampuni kwenye maeneo ya Bahari kwa Zanzibar.

DKT. MWINYI AMEPOKEA SALAMA ZA POLE KUTOKA KWA KAMPUNI YA WASAFI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyiamepokea Salama za Pole kutoka kwa Kampuni ya Wasafi inayoongozwa na Mkurugenzi mkuu, Nasib Abdul (Daimond Platnum).

Dkt. Mwinyi alipokea salamu hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Kiongozi huyo na Wajumbe aliofuatana nao ameushukuru Uongozi wa Wasafi uliofika kwa lengo la kumfariji kufuatia Msiba wa Baba yake Mzazi, Mzee Ali Hassani Mwinyi.

RAIS MWINYI AMETOA SHUKRANI KWA WANANCHI WA TAASISI ZOTE ZILIZOMUOMBEA DUA MZEE ALI HASSAN MWINYI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa Shukrani kwa wale wote wanaomuombea Dua Marehemu Rais Mstaafu wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi tokea alipofariki Tarehe, 29 Februari 2024 hadi leo.

DKT. HUSSEIN MWINYI AMEPOKEA SALAMU ZA POLE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea Salamu za Pole  kwa Viongozi Wakuu na Viongozi Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Viongozi wa Vyama vya siasa.

Waliotoa Salam za Pole ni Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Mashaka Biteko, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi

DKT. MWINYI AMEFARAJIKA NA JUMUIYA YA VETERAN YOUNG PIONEERS

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema amefarajika kuona Jumuiya Veteran Young Pioneers Zanzibar inapongeza utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika kipindi cha Miaka Mitatu.

Akizungumza na Maveterani hao Ikulu Jijini Zanzibar amesema pongezi hizo zitakua chachu ya kuongeza kasi katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo.

Aidha Dkt. Mwinyi ameipongeza Jumuiya hiyo kwa kuendeleza Majukumu yao ya kujitolea, kuwafundisha Vijana Uzalendo, ukakamavu na itikadi ya Chama.

WAFANYABIASHARA WAMETAKIWA KUACHA KUPANDISHA BEI KIHOLELA

Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amewataka Wafanyabiashara kushirikiana na Serikali katika kuzingatia Bei za Bidhaa zao hasa katika Kipindi hiki cha kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea baadhi ya Masoko na Maeneo ya Biashara amesema Serikali itafanya kila iwezalo kuwasaidia Wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuwapunguzia ushuru kwa Bidhaa zinazotoka Nje ya Nchi ambazo ni muhimu ikiwemo Sukari ili kuhakikisha Wananchi wanamudu Maisha katika kipindi hicho.

Subscribe to DKT HUSSEIN ALI MWINYI
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.