SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MIUNDOMBINU KATIKA MAENEO YA UTALII

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Hussein Ali Mwinyi  amesema Serikali itaendela kujenga Miundombinu  katika maeneo ya Utalii  ili Wananchi waweze  kufanya shughuli zao kwa  uhakika.

Akifungua Mkutano wa pili wa Wadau wanaouza Bidhaa za Utalii kutoka Nchi mbali mbali Duniani, huko Golden Tulip Uwanja wa Ndege,amesema Miundo Mbinu hiyo itaongeza ukuaji wa Uchumi na pato la Taifa.

RAIS MWINYI AFUNGUA MKUTANO MKUU ZNCC

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka Wafanyabiashara kuendesha biashara zao kwa kuzingatia misingi ya haki na uadilifu na kulipa kodi ili Serikali iweze kukusanya Mapato na kuendelea kutoa huduma bora kwa Jamii.

DKT. MWINYI ATOA POLE KWA MSIBA WA EDWARD LOWASSA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameungana na Viongozi wa Chama, Serikali na wakaazi wa Jiji la Dar Es Salaam kutoa Mkono wa pole katika Msiba wa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowasa.

Akiwa ameambatana na Mkewe Mama Maryam Mwinyi Raisi Mwinyi amemuelezea Hayati Edward Lowasa kuwa ni Kiongozi

UWEKEZAJI UNAHITAJI KUWEPO KWA MIFUMO IMARA YA UTOAJI HAKI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema uwekezaji wa Miradi ya Kiuchumi unahitaji uwepo Mifumo imara wa utoaji haki.

ZANZIBAR YAPONGEZWA KWA KUIMARISHA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi mdogo wa China Mhe. Zhang Zhisheng anayefanyia kazi zake Zanzibar, kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi Nchini.

Rais Dk Mwinyi amemshukuru Balozi Zhang kwa kudumisha na kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Zanzibar na China katika miaka mitatu ya utumishi wake Nchini.

DKT HUSSEIN ALI MWINYI AMEPONGEZWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WALIOFIKA IKULU ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amepongezwa na Viongozi mbalimbali waliofika Ikulu Zanzibar kwa sherehe zilizofanywa za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Majeshi ya ulinzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania CDF Jenerali Jacob John Mkunda alipokutana na kufanya mazunguzu na Dkt Mwinyi Ikulu.

VIONGOZI WA JUMUIYA YA UMOJA WA VIJANA UVCCM KATIKA HAFLA YA CHAKULA CHA USIKU

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi amejumuika pamoja na Viongozi  wa jumuiya ya umoja wa Vijana UVCCM katika hafla ya Chakula cha usiku

Akizungumza na Vijana  katika hafla hiyo Rais Dk.Mwinyi amesema

Serikali na Chama cha Mapinduzi wamefarajika  kwa kuungwa mkono katika sherehe  za miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya

Zanzibar.

UCHUMI WA NCHI YOYOTE DUNIANI HAUWEZI KUJENGWA NA SEKTA YA UMMA PEKEE BALI NI LAZIMA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema uchumi wa Nchi yoyote Duniani hauwezi kujengwa na Sekta ya umma pekee bali ni lazima kushirikiana na Sekta Binafsi katika uwekezaji wa Miradi mbali mbali ya Kiuchumi.

DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEELEZEA KURIDHISHWA NA VIWANGO VYA UJENZI WA BARABARA YA UWANJA WA NDEGE-MNAZIMMOJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dkt. Hussein Ali Mwinyi ameelezea kuridhishwa na viwango vya ujenzi wa Barabara ya Uwanja wa Ndege-Mnazimmoja amesema kuwa itakuwa ya mfano na inaendana na kasi ya ukuaji uchumi wa Zanzibar.

Dkt. Mwinyi akizungumza katika uwekaji Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Bara Bara hiyo   yenye urefu wa Kilomita 6 nukta 8, amesema Serikali lengo la Serikali ni kuona Barabara zote zinajengwa kwa kiwango bora ili zitumike kwa muda mrefu huku akiwataka Wanachi kuacha kufanya Biashara pembezoni mwa Barabara.

Subscribe to DKT HUSSEIN ALI MWINYI
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.