Habari

WAMAREKANI WAKARIBISHWA KUEKEZA ZANZIBAR

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina fursa nyingi za Uwekezaji hivyo amewataka Wawekezaji kutoka Marekani wazitumie fursa hizo kwa kuekeza Zanzibar.

    Dkt. Mwinyi ameyasema hayo huko Ikulu wakati alipotembelewa na Wabunge wa Bunge la Senate la Marekani, amesema Serikali imeipa kipaumbele Sekta ya Uchumi wa Buluu kwani ni moja ya Eneo linatoa fursa nyingi za Ajira kwa Jamii

UJENZI WA VIWANJA VYA NDEGE NI FURSA ZA KUONGEZEKA PATO LA NCHI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Viwanja vya Ndege ni sehemu ya ukuwaji wa uchumi wa Zanzibar ambayo inategemea zaidi shughuli za Utalii ambazo zinakwenda sambamba na uwepo wa Miundombinu mizuri ya Viwanja hivyo. 

Ameyasema hayo wakati alipofanya Ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbali mbali inayojengwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibari. 

WAKULIMA WA MWANI KUWEZESHWA ILI KUJIKWAMUA NA KIMAISHA

Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Kisiwani Pemba imesema itaendelea kushirikiana na Mashirika mbali mbalikwa kuwajengea uwezo Wakulima wa Mwani ili waweze kujikwamua Kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Kitengo cha Mwani Bi Hidaya Khamis Hamad mara baada ya kukamilika kwa Mafunzo ya Wakulima wa Mwani kupitia Mradi wa  Ifad yaliyofanyika  katika Ukumbi wa Makonyo  Wawi Chakechake Pemba ,

ZURA KUTOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA KANUNI ZA UTOAJI VIBALI KWA MAFUNDI UMEME.

Mamlaka ya kudhibiti huduma za Maji Nishati (Zura) imeshauriwa kutoa ELimu kwa Watumiaji wa Kanuni ya utoaji vibali kwa Mafundi Umeme umuhimu wa kuwepo  Kanuni hiyo na utekelezaji wake.

Ikipopokea maoni ya Watumiaji wa Kanuni hiyo katika kamati ya Kanuni na Sheria ndogo ndogo ya Baraza la Wawakilishi chini ya kaimu Mwenyekiti Mhe.Mwanaasha Khamis Juma huko Maisara imebaini kuwa baadhi ya Watumiaji wa kanuni hiyo hawana uelewa kuwa tayari kanuni hiyo imeanza kutumika na kusababisha kuwepo kwa mapungufu katika utekelezaji wake.

KUKAMILIKA UJENZI KATIKA TERMINAL ONE NA TWO ITAONDOWA CHANGAMOTO YA MSONGAMANO KATIKA TERMINAL THREE

     Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Viwanja vya ndege ni sehemu muhimu sana kwa ukuwaji wa uchumi wa Zanzibar ambayo inategemea zaidi shuhuli za utalii ambazo zinakwenda sambamba na uwepo wa miundombinu mizuri ya viwanja hivyo.

     Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbali mbali inayojengwa na Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibari.

SERIKALI KULIPA FIDIA KWA WANANCHI WATAKAOATHIRIWA VIPANDO VYAO KUPISHA UJENZI CHUMBUNI

    Serikali italipa fidia  Wananchi  vipando vyao vimeathiriwa kwa kupisha  Ujenzi wa Nyumba za Gharama nafuu katika  Eneo la Chumbuni.

    Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Salha Mwinjuma amesema inaendelea na kutathamini katika Eneo hilo na Wananchi wote watalipwa  fidia  zao kulingana na miongozo na kanuni ziliopo.

SERIKALI YAJIPANGA KUIMARISHA SEKTA YA UVUVI KATIKA HUBA YA CHWAKA

    Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi  na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kusini Unguja wameweka adhimio la kutokomeza Uvuvi haramu katika Huba ya Chwaka.

    Kufuatia  kutumia dhana haramu katika shughuli za Uvuvi  Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe.Shaabani Ali Othman amesema Serikali imekusudia kutoa Boti Mia Moja za Kisasa ambazo zitakuwa na dhana kamili za Uvuvi zitakazowawezesha Wavuvi kufika kina kirefu cha Maji na kuondokana na Uvuvi haramu. 

JESHI LA POLISI WAOMBA WAZAZI KUSIMAMIA VIZURI SUALA LA MALEZI ILI KUJENGA TAIFA BORA

     Jeshi la Polisi limeiomba Jamii na kuikumbusha kujikitaka katika malezi kwa watoto ili kujenga jamii inayochukia uhalifu na yenye hofu ya Mungu huku Jeshi hilo likiwaomba wananchi kutoa taarifa za uhalifu na ukatili katika Jamii.

     Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es salaam katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu katoliki la Dar es salaam na Mkuu wa Polisi Jamii kituo cha Polisi Kati Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Rose Mbaga alipokuwa akitoa Elimu kwa waumini walio hudhuria ibada hiyo .

MSAKO MKALI KUFANYIKA KWA WASIO RIPOTI KIDATO CHA KWANZA WILAYA YA MASASI

     Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Lauteri John Kanoni amewapatia taarifa wakazi wa Masasi kuhusu wazazi wasiopeleka wanafunzi kidato cha kwanza Mwaka huu Serikali inawachukulia hatua kali na msako huo unaanza 15/7/2024.

     Endapo mwanafunzi ni mjamzito kwa aliempa ujauzito atachukuliwa hatua Kali za kisheria na mwanafunzi akijifungua anatakiwa kurudi Shuleni na kuendelea na masomo kama kafariki basi mzazi atalazimika kuonesha udhibitisho kwa kuonesha cheti cha kifo

WEMA NA KAMPUNI YA UJENZI UNITED RUMP KUKABIDHI ENEO LA UJENZI WA DAHALIA PEMBA

   Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imefanya Makabidhiano ya Eneo la Ujenzi wa Dahalia na Kampuni ya Ujenzi United Rump katika Chuo cha Kiislam Pemba .

   Katika makabidhiano hayo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.Lela Mohd Mussa amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya United Rump kuharakisha Ujenzi wa Dahalia katika  Chuo hicho ili Wanafunzi waweze kuondokana na Usumbufu wanaoupata .

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.