ZURA KUTOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA KANUNI ZA UTOAJI VIBALI KWA MAFUNDI UMEME.

ZURA

Mamlaka ya kudhibiti huduma za Maji Nishati (Zura) imeshauriwa kutoa ELimu kwa Watumiaji wa Kanuni ya utoaji vibali kwa Mafundi Umeme umuhimu wa kuwepo  Kanuni hiyo na utekelezaji wake.

Ikipopokea maoni ya Watumiaji wa Kanuni hiyo katika kamati ya Kanuni na Sheria ndogo ndogo ya Baraza la Wawakilishi chini ya kaimu Mwenyekiti Mhe.Mwanaasha Khamis Juma huko Maisara imebaini kuwa baadhi ya Watumiaji wa kanuni hiyo hawana uelewa kuwa tayari kanuni hiyo imeanza kutumika na kusababisha kuwepo kwa mapungufu katika utekelezaji wake.

Wajumbe wa Kamati hiyo wamesisitiza kuharakisha kutolewa kwa elimu hiyo kwa Watumiaji ambapo kutasaidia kupunguza udanganyifu wa baadhi ya watendaji wasio na maadili.

Msaidizi Mkurugenzi Umeme Haji Silima Haji na Mkurugenzi Sheria Rashid Abdulla Fadhil wamesema watahakikisha wanayapatia ufumbuzi mapungufu yaliyojitokeza kwa  lengo la kuisadia Jamii kupata huduma bora ya Umeme. 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.