Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Kisiwani Pemba imesema itaendelea kushirikiana na Mashirika mbali mbalikwa kuwajengea uwezo Wakulima wa Mwani ili waweze kujikwamua Kiuchumi.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Kitengo cha Mwani Bi Hidaya Khamis Hamad mara baada ya kukamilika kwa Mafunzo ya Wakulima wa Mwani kupitia Mradi wa Ifad yaliyofanyika katika Ukumbi wa Makonyo Wawi Chakechake Pemba ,
Amesema lengo la Mafunzo hayo nikuwaona Wakulima wa Mwani wananufaika na Mazao yatokanayo Bahari ili kuenda Sambamba na Sera ya Uchumi wa Buluu.
kwa upande wao, Wakulima waliopatiwa Mafunzo hayo wamesema kupatiwa kwa Taaluma hiyo ya Mbinu mpya ya ukulima wa Mwani itasidia kuleta mabadiliko katika shuhuli zao huku wakishukuru Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi nakueleza matatizo wanayokutana nayo.
Mapema akiwasilisha mada afisa kutoka Wizara ya uchumi wa Buluu na Uvuvi Kitengo cha Mwani , Aisha Khamis Sultan amewataka wakulima hao kufanya utafiti kabla ya kuanza shuhuli za Kilimo sambamba, kuchukua tahahadhari pindi wanapokuwa katika shuhuli zao.