Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kusini Unguja wameweka adhimio la kutokomeza Uvuvi haramu katika Huba ya Chwaka.
Kufuatia kutumia dhana haramu katika shughuli za Uvuvi Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe.Shaabani Ali Othman amesema Serikali imekusudia kutoa Boti Mia Moja za Kisasa ambazo zitakuwa na dhana kamili za Uvuvi zitakazowawezesha Wavuvi kufika kina kirefu cha Maji na kuondokana na Uvuvi haramu.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhammed Mahamoud amesema Mkoa unaunga mkono adhimio hilo ambalo litaleta tija kwa Wananchi na ameomba kufata Sheria na Kanuni zinazowekwa.
Walioshiriki katika Kikao hicho wameridhishwa na mpango huo ambao utasaidia Wavuvi na wameomba kuongeza kuwapatia Elimu.