Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Lauteri John Kanoni amewapatia taarifa wakazi wa Masasi kuhusu wazazi wasiopeleka wanafunzi kidato cha kwanza Mwaka huu Serikali inawachukulia hatua kali na msako huo unaanza 15/7/2024.
Endapo mwanafunzi ni mjamzito kwa aliempa ujauzito atachukuliwa hatua Kali za kisheria na mwanafunzi akijifungua anatakiwa kurudi Shuleni na kuendelea na masomo kama kafariki basi mzazi atalazimika kuonesha udhibitisho kwa kuonesha cheti cha kifo
Aidha Kanoni amesema kuanzia 15/7/2024 ugawaji wa pembejeo kwa wakulima utasimamiwa vizuri na wataalam wa kilimo Kwa kushirikiana na watendaji kata, vijiji na bodi ya korosho
Kanoni ameyasema hayo katika kikao na viongozi wa CCM Wilayani Masasi na hayo yote ni katika kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.