UJENZI WA VIWANJA VYA NDEGE NI FURSA ZA KUONGEZEKA PATO LA NCHI

MAKAMO WA PILI WA RAIS

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Viwanja vya Ndege ni sehemu ya ukuwaji wa uchumi wa Zanzibar ambayo inategemea zaidi shughuli za Utalii ambazo zinakwenda sambamba na uwepo wa Miundombinu mizuri ya Viwanja hivyo. 

Ameyasema hayo wakati alipofanya Ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbali mbali inayojengwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibari. 

Mhe. Hemed amesema kuwa Viwanja vya Ndege ni Milango Mikuu ya Nchi yoyote ile Duniani inayotumika kwa kusafirishia Wageni ambao huchangia kukuwa kwa Uchumi na kuongezeka kwa pato la Nchi husika

Aidha amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikano kwa Kampuni zinazojenga Miradi mbali mbali Nchini ikiwemo Kampuni ya Estim Constraction LTD ili kuhakikisha wanakabidhi Miradi kwa wakati uliopangwa

Waziri wa Ujenzi, mawasiliano na usafirishaji Dkt Khalid Salum Muhamed amesema Uchumi wa Zanzibar unategemea zaidi Utalii hivyo ni lazima kuimarisha miundombinu ya kimkakati ikiwemo viwanja vya Ndege ili kuhakikisha utalii unakuwa kwa kasi na pato la nchi linaongezeka kupitia Wagemi wanaoingia Zanzibar.  Nae mshauri elekezi kutoka Kampuni ya anova Consult LTD Muhandisi  Ibrahim Gasper amesema hadi sasa Miradi ipo vizuri na kuahidi kukamilika na kukabidhi Miradi hiyo ndani ya muda uliopangwa na kwa kuzingatia viwango.

 katika ziara hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amekagua matengenezo ya jengo la Terminal one, Ujenzi wa gengo la terminal two pamoja na Ujenzi wa sehemu ya Biashara iliyopo Terminal Three. 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.