Habari

SGR KUANZA SAFARI YA KWANZA DAR HADI DODOMA

    Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanza Safari ya Kwanza ya Treni ya Kisasa ya SGR kutoka Dar es salaam hadi Dodoma ambapo imeondoka Majira ya Saa 12 Alfajiri Jijini Dares salaam.

      Akizungumza wakati wa Safari hiyo Jijini Dar- es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Masanja Kadogosa amesema kuanza kwa Safari hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia la kutaka ifikapo Mwishoni mwa Mwezi wa Julai Treni hiyo ianze kufanya Safari zake.

ZANZIBAR KUTOA BIMA YA AFYA KWA WAGENI

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Fedha na Mipango Dk. Saada Mkuya Salum amesema Serikali imetayarisha huduma za Bima  kwa wageni wanaoingia Zanzibar inayotarajia kuanza septemba mwaka huu.

Akizungumza na Wadau wa usafiri wa Mashirika ya Ndege ya Nje na ndani ya Nchi amesema Taratibu zinaendelea kukamilika na Bima hiyo itasisha huduma za Afya na nyingine wakati wote anapokuwa Nchini.

Amesema Serikali inaendelea kuimarisha huduma za Afya na Miundombinu ya Kiuchumi ili kuona Zanzibar inakuwa sehemu Nzuri ya kufikia Wageni.

MABARAZA YA MANISPAA KUWAONDOA WAFANYA BIASHARA NA WAENDESHA BODA BODA SEHEMU ZISIZO RASMI

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Idrisa Kitwana Mustafa ametoa muda wa Siku Tatu kwa Mabaraza ya Manispaa ndani ya Mkoa huo kuwaondoa Wafanya Biashara na waendesha Boda Boda kwenye maeneo yasio rasmi ya Watembea kwa Miguu ili kuhakikisha Mji unakuwa na haiba nzuri.

Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza na  Vyombo vya habari kuhusiana na Operesheni huo amesema ni marufuku kuendesha Gari na Vyombo vya moto vyengine   katika    Njia za watembea kwa miguu ili kupunguza Ajali za Barabarani zinazojitokeza mara kwa mara .

WIZARA YA AFYA KUSHIRIKIANA NA CHINA KUIMARISHA TAFITI ZA AFYA

Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe Nassor Ahmed Mazrui amesema watashirikina na Chuo Kikuu cha Fudan Medical cha Shanghai Nchini China kwa masula tafiti na Taaluma za Afya.

Ameyaeleza hayo alipozungumza na ujumbe kutoka Chuo Kikuu hicho ambao umefika Nchini amesema hivi sasa Wizara ya Afya ina Mkataba wa kuimarisha masuala ya tafiti kupitia Taasisi ya utafiti zahri Binguni na katika kuendelea hilo Watasaini Mkataba na Chuo hicho.

Amefahamisha kuwa kuja kwa ujumbe huo kutasaidia kuongeza mambo mbali mbali ya kuimarisha Sekta afya ambayo yatahusika katika Mkataba huo. 

MAMLAKA MOROGORO KUONDOA MAJANI YALIOOTA BWAWA LA MINDU

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ameitaka Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira na Bodi ya Maji, Bonde la Wami Ruvu kushirikiana kuondoa Majani ambayo yaliyoota juu ya Maji ya Bwawa la Mindu lililopo Manispaa ya Morogoro ambalo linategemewa na wakazi wa Manispaa hiyo.

Mheshimiwa Aweso ametoa maelekezo hayo wakati wa Ziara yake ya Siku Moja Mkoani morogoro ya kutembele Bwawa hilo na kushuhudia Majani ambayo yameota juu ya Maji huku shughuli za kuyaondoa zikiendelea.

SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU NA WAFADHILI WA NDANI NA NJE YA NCHI

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Leila Mohammed Mussan amesema wataendelea kushirikiana na Wadau na wafadhili wa ndani na Nje ya Nchi kwa lengo la  kukuza Sekta za Elimu ya juu   ili kupata Wataalamu wa baadae.

WANANCHI WILAYA YA MBINGA WASHAURIWA KUTUMIA NISHATI SAFI KWA LENGO LA KUHIFADHI MAZINGIRA

    Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wametakiwa kutumia fursa zitokanazo na uwepo wa nishati ya makaa ya mawe ili kujinusuru na changamoto za kiafya na za uhifadhi mazingira

     Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kisare Makori wakati wa hafla ya ugawaji wa tani 10 za nishati mbadala itokanayo na makaa ya kwa shule za msingi 15 pamoja na sekondari 15 kwa ajili ya kupikia

SOKO KUU WILAYA YA MASASI LATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO

     Soko Kuu la Mji Masasi (Mkuti) limeteketea kwa Moto usiku wa kuamkia leo Julai 17,2024 kuanzia majira ya saa 4 usiku na kuathiri upande wa eneo la Mauzo ya Samaki pamoja na kusababisha hasara kubwa kwa Wafanyabiashara wa Soko hilo.

      Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Maafisa Uchunguzi wa Maafa bado hawajatoa taarifa kamili kuhusu chanzo cha Moto huo japo mashuhuda wameeleza kuwa ni Shoti ya Umeme ambapo ni baada ya umeme kukatika na kurudi kwa nguvu kubwa na kushindwa kuuhimili

MIUNDOMBINU YA UMEME KUTOA FURSA KWA WAWEKEZAJI

    Wizara ya Maji, Nishati na Madini imetiliana Saini Hati ya Makubaliano na Kampuni Mbili kutoka Nchini China kwa ajili ya   Mkataba wa Kazi ya Ujenzi wa Miundo mbinu ya Umeme.

    Akizungumza katika Hafla ya Utiaji Saini huo Waziri wa Maji Nishati na Madini Mhe.Shaibu Hassan Kaduara amesema Mradi huo wa kupitisha laini za Umeme na kupoozea Umeme huko Makunduchi na Matemwe  utaisaidia Zanzibar kuondokana na tatizo la Umeme mdogo pamoja na upotevu wa Umeme unaojitokeza katika Maeneo mbalimbali.

DKT. SAMIA AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MIRADI

      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi Mkoani Rukwa kutunza Miradi inayojengwa kwenye Maeneo yao ili iweze kudumu na kuleta tija ya fedha zinazotumika kukamilisha Miradi hiyo.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.