Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Leila Mohammed Mussan amesema wataendelea kushirikiana na Wadau na wafadhili wa ndani na Nje ya Nchi kwa lengo la kukuza Sekta za Elimu ya juu ili kupata Wataalamu wa baadae.
Akizungumza na Wadau mbalimbali huko Chuo iit Madrasa Compas Bweleo amesema ushirikiano huo itasaidia kupiga hatua za kimaendeleo na kutoa fursa kwa Vijana wasomi ili kujikuza Kielimu na kuiletea Mandeleo Serekali na kuwasisitiza Wanafunzi wa chuo hicho kuongeza juhudi katika masomo yao ili Wadau hao waweze kuwaunga Mkono
Nao Wadau hao wamesema Wataendendeleza ushirikiano na kukisaidia Chuo hicho pamoja na Wanafunzi hasa wale wenye uwezo mdogo ili kujiendeleza Kielimu
Zaidi ya Shilingi Bilioni Mbili za Kitanzania zimetolewa na Kampuni mbalimbali kwa ajili ada ya Wanafunzi na maendeleo ya Chuo.