Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe Nassor Ahmed Mazrui amesema watashirikina na Chuo Kikuu cha Fudan Medical cha Shanghai Nchini China kwa masula tafiti na Taaluma za Afya.
Ameyaeleza hayo alipozungumza na ujumbe kutoka Chuo Kikuu hicho ambao umefika Nchini amesema hivi sasa Wizara ya Afya ina Mkataba wa kuimarisha masuala ya tafiti kupitia Taasisi ya utafiti zahri Binguni na katika kuendelea hilo Watasaini Mkataba na Chuo hicho.
Amefahamisha kuwa kuja kwa ujumbe huo kutasaidia kuongeza mambo mbali mbali ya kuimarisha Sekta afya ambayo yatahusika katika Mkataba huo.
Mkuu wa Chuo cha Fudan Medical Zhenghoug Yuan amesema lengo la kuja Zanzibar ni kuimarisha ushirikino uliopo baina ya nchi hizo mbili kwa kuimarisha tafiti za kiafya na masomo kwa Wafanyakazi.
Zanzibar na China ina uhusiano tokea Mwaka 1964 na inasadia katika Sekta mbali mbali ikiwemo afya kwa kuwapatia Madaktari wa kutoa huduma Unguja na Pemba.