WANANCHI WILAYA YA MBINGA WASHAURIWA KUTUMIA NISHATI SAFI KWA LENGO LA KUHIFADHI MAZINGIRA

Halmashauri Wilaya ya Mbinga

    Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wametakiwa kutumia fursa zitokanazo na uwepo wa nishati ya makaa ya mawe ili kujinusuru na changamoto za kiafya na za uhifadhi mazingira

     Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kisare Makori wakati wa hafla ya ugawaji wa tani 10 za nishati mbadala itokanayo na makaa ya kwa shule za msingi 15 pamoja na sekondari 15 kwa ajili ya kupikia

    Makiro ameipongeza Halmashauri hiyo kwa uamuzi wa kutumia nishati safi kwani takwimu zinaonyesha zaidi ya hekta mia tisa za miti sawa na miti milioni moja na elfu thelathini ukatwa kila mwaka  kwa matumizi ya kupikia.

     Amesema Serikali inaunga mkono sera mbalimbali za kimataifa kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia na uhifadhi mazingira ili kupunguza matumizi ya nishati chafu na isiyo salama katika Nyanja za kijamii, kiuchumi, kiafya na kimazingira

    “Niwapongeze kikundi cha Wanawake Mbalawala ambao ni wanufaika wa mkopo wa 10% kwa ubunifu na kutumia fursa zilizopo katika kuunga mkono juhudi za serikali katika matumizi ya nishati mbadala ambayo ni chachu katika kuhifadhi mazingira”amisema DC Makiro

     Pia amesema ili biashara ya kukata kuni na matumizi ya mkaa yafike kikomo ni lazima wananchi wabadilike kwa kuacha kukata miti hivyo pia amewataka viongozi wa taasisi na wadau kuendelea na juhudi za  upandaji miti na kupinga shughuli za kilimo kwenye vyanzo vya maji

     Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga Joseph Rwiza amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha katika kata zote kupitia viongozi ili wateo elimu ya nishati safi kwa wananchi ikiwemo na sehemu zinazo hudumia watu wengi kama vile mashuleni lengo

    “Nimejipanga katika Halmashauri yetu kuhakikisha shule zetu zote za msingi na sekondari tunalisimamia ndani ya muda mfupi kuanza kutumia nishati mbadala ya makaa ya mawe ili kuhakikisha zoezi linakuwa endelevu na kuunga mkono wazalishaji wetu wa nishati safi” amesema Rwiza

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.