Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanza Safari ya Kwanza ya Treni ya Kisasa ya SGR kutoka Dar es salaam hadi Dodoma ambapo imeondoka Majira ya Saa 12 Alfajiri Jijini Dares salaam.
Akizungumza wakati wa Safari hiyo Jijini Dar- es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Masanja Kadogosa amesema kuanza kwa Safari hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia la kutaka ifikapo Mwishoni mwa Mwezi wa Julai Treni hiyo ianze kufanya Safari zake.
Amesema zaidi ya Abiria Mia Tisa wamefanikiwa kusafiri na Treni ya Mwendo kasi SGR ikiwa ni katika Safari zake ambazo zimeanza Tasmi Leo Julai 25 2024, na kutumia Mabehewa Kumi na Nne na kuwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kwa kutumia.
Miongoni mwa Abiria ambao wamesafiri kwa Mara ya Kwanza na Treni ya SGR wameeleza kufurahishwa na huduma hiyo kwani ni
Rafiki na kumfanya Mtu Asafiri kwa Amani, Haraka na Uhakika.
Safari ya Treni ya SGR kutoka Dar es salaam Hadi Dodoma imeanza ikiwa ni Mwezi Mmoja na Siku 11 Tangu kuanza kwa Safari zake kutoka Dar es salaam hadi Morogoro zilizoanza Juni 14 2024, ambapo Raisi Samia anatarajiwa kuzinduwa Rasmi wa Safari za kutoka Dar hadi Dodoma hivi Karibuni.