Habari

MRADI WA KUSAFIRISHA UMEME KUTOKA IRINGA-SUMBAWANGA KUINUA UCHUMI WA WANANCHI

Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Mashaka Biteko ameweka jiwe la msingi katika Mradi wa kusafirisha Umeme Kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzaniaa na Zambia(TAZA) hatua itakayosaidia kuinua Uchumi kupitia Nishati.

UZINI IMEIOMBA KUTENGENEZEWA MIUNDOMBINU YA SKULI

Kamati ya Skuli ya Msingi Uzini imeiomba Serikali kutengeneza  Miundombinu  ya Skuli hiyo kutokana  na kuchakaa jambo linalosababisha usumbufu kwa Wanafunzi wakati wa kusoma.

Akizungumza katika ziara ya kukagua  Skuli hiyo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdul-Gulam Hussein ambapo amesema uchakavu wa Miundombinu hiyo imekuwa tatizo la muda mrefu hali inayosababisha kutokupata huduma za msingi inayohatarisha ubora wa kiwango cha Elimu.

MECCO IMEHIMIZWA KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA CHAKE-WETE

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amemuhimiza Mkandarasi wa kampuni ya Ujenzi ya Mecco inayojenga barabara ya Chake-Wete, kufanya uharaka wa kukamilisha Ujenzi wa Barabara hiyo ili kujenga imani ya Wananchi na kuwaondolea usumbufu.

TUME YA HAKI ZA BINAADAMU KUIMARISHA MPANGO KAZI WA KIBIASHARA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria utumishi na Utawala bora Mh Haroun Ali Suleiman ameitaka Tume ya haki za Binaadamu na utawala bora Tanzania kuwa makini katika kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu  utekelezaji wa mpango kazi wa haki za Binaadamu na Biashara Zanzibar.

Akizungumza na Watendaji wa Tume hiyo huko Ofisini kwake Mazizini amesema kufikia malengo la Ziara hiyo ni kutafuta maoni ya Wananchi wenyewe badala ya Viongozi ili kufanikisha vyema mpango huo

DKT.NCHIMBI AZURU KABURI LA HAYATI MKAPA

     Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ametembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya 3, hayati Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso mkoani Mtwara, leo Julai 28, 2024, kuhani familia na kuzungumza na wananchi wa Lupaso.

DKT.MWINYI AITAKA JAMII KUHAKIKISHA WANASIMAMIA VYEMA MAADILI KWA WATOTO NA VIJANA

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amehimiza Malezi bora katika Jamii na kuhakikisha wanasimamia  vyema  maadili kwa Watoto na  Vijana ili kunusuru Taifa.

     Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati  akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya Ibada ya Sala ya Ijumaa

iliyofanyika Masjid Taqwa  Mwanakwerekwe Meli Nne Wilaya ya Magharibi 'b' Mkoa wa Mjini Magharibi.

MAKAMO WA PILI WA RAIS AONGOZA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KUMSALIA MAREHEMU AMOUR KHALFAN

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na Viongozi wa Serikali,  Wanafamilia na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Swala na Dua ya kumuombea Marehemu Amour Khalfan Salum aliekuwa Mtangazaji Mstaafu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC)

     Marehemu Amour Khalfan amesaliwa Msikiti wa Muembe Tanga Wilaya ya Mjini na kuzikwa Kijijini kwao Kianga.

 Inna Liilahi Wainna Ilaihi Raajiun.

RAIS SAMIA AONGOZA WATANZANIA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu  Dkt. Samia Suluhu Hassan   Amewaongoza  Viongozi mbalimbli akiwemo  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.  Hussein Ali Mwinyi katika  Siku ya  Kumbukumbu ya Mashujaa  Waliopigania Uhuru wa Tanzania katika  Mji wa Serikali Mtumba Jijini  Dodoma. 

HOFU YAWAJAA WAKAAZI WA KARAKARA KUTOKANA NA JAA LILOPO KATIKA ENEO LAO

    Kuwepo Jaa kubwa katika Eneo la Karakana ambalo ni Makaazi ya Watu pamoja Wafanyabiashara, limetajwa kuwa Tishio na usalama wa Afya zao.

    Jaa hilo ambalo kwa mujibu wa Wafanyabiashara wa Eneo hilo, wamesema linakadiriwa kuwepo kwa Miezi Mitatu bila ya kuchukuliwa Taka hizo, linaleta hofu kutokana na harufu inayosambaa pamoja na Wadudu na kukwamisha Biashara.

ZBC IMETIA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA SHIRIKA LA UTANGAZAJI COMORO

    Katika kuendeleza Ushirikiano wa Zaidi ya Miaka 15 kati ya Tanzania na Comoro, Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) limetia Saini Mkataba wa Ushirikiano na Shirika la Utangazaji Comoro ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu. 

    Kwa upande wa ZBC Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Ndg.Ramadhani Bukini na kwa upande wa Comoro amesaini Balozi wa Comoro Nchini Tanzani Dkt.Ahmada Mohammed.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.