Habari

WALIMU WAMETAKIWA KUUTUMIA MTAALA MPYA ILI KUONGEZA UFAULU

Wizara ya ELimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imewataka Walimu wa Skuli zote kuufuata Mtaala mpya wa Elimu ikiwemo kuwasomesha Wanafunzi Vitabu ili kuvifahamu, kufauli vizuri mitihani pamoja na kuwa na kuelewa wa Stadi za maisha.

MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO IMEHAMISHIWA OFISI YA RAIS IKULU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mhe Ali Suleiman Ameir amewataka Viongozi na Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao kuhakikisha kuwa inayaendeleza mazuri yaliyokuwa yakifanyika kabla ya kuhamia Ofisi ya Rais Ikulu.

Waziri Mrembo ameyasema hayo huko Mazizini alipokuwa akijitambulisha Rasmi kwa Viongozi na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Serikali mtandao baada ya Mamlaka hiyo kuhamishwa kutoka Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora na kuingizwa katika usimamizi wa Ofisi ya Rais Ikulu. 

MAAFISA USAFIRISHAJI DODOMA WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA SGR

   Maafisa usafirishaji Mkoa wa Dodoma wametakiwa kutumia vyema fursa ya Ujio wa Treni ya Kisasa kwa kuhakikisha wanalinda Picha ya Serikali kwa kuwafikisha salama Abiria watakaotumia Treni hiyo.

    Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea Uzinduzi Rasmi wa Safari za Treni ya Umeme, itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Agosti Mosi Mwaka huu katika Stesheni kuu Dodoma. 

KAMISHENI YA WAKFU YALALAMIKIWA UCHELEWESHAJI WA UGAWAJI WA MIRATHI

     Familia ya Juma Issa Noura imeilalamikia Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar kwa kile Wanachodai kukwamishwa kwa Mpango wa ugawaji wa Mirathi inayotokana na mali zilizoachwa na Baba yao. 

    ZBC imezungumza na Mussa Juma Issa ambae ni Mtoto kati ya Watoto Watano wa Marehemu Juma Issa Noura ambae ni msimamizi wa Mirathi hiyo yenye Jarada Namba Nne Mwaka 2009 

DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ANATARAJIA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI MOROGORO
NANI KUTEULIWA NAFASI YA KINANA BAADA YA KUJIUZULU?

    Maswali yamekuwa mengi baada ya kutoka Taarifa ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama tawala Tanzania Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulraman Kinana, kujiuzulu.

    Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama tawala CCM Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana.

MH.MAJAALIWA AFUNGUA KONGAMANO LA MAENDELEO YA SEKTA YA AFYA

      Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiambatana na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui wakitembelea na kukagua mabanda ya wadhamini pamoja na wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya baada ya kuwasili kwenye Kongamano linalofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam.

WAZIRI SILAA ATEMBELEA OFISI ZA TCRA

     Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb) ametembelea ofisi za makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zilizoko jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Kuwe.

     Waziri Silaa amefanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza na kupitishwa kwenye majukumu yanayotekelezwa na mamlaka hiyo na namna wanavyoshughulikia masuala ya Habari na Mawasiliano.

SERIKALI MTANDAO YATAKIWA KUHAKIKISHA SERIKALI INATUMIA MIFUMO YA KIELEKTRONIKI

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Mhe. Ali Suleiman Ameir ameitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao kuhakikisha kuwa Serikali inafanikiwa kutumia mifumo ya kieletroniki, kuwa na uwazi katika kutekeleza majukumu ya kila siku na kuhakikisha inatimiza jukumu la kuziunganisha Taasisi mbali mbali za Serikali katika mifumo ya kiserikali.

UCHUMI WA TANZANIA UMEENDELEA KUKUA KWA ASILIMIA TANO NUKTA MBILI

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesetoa wito kwa Wadau wa Sekta Binafsi kushirikiana Serikali kuekeza katika Miradi ya ubia kati ya Sekta ya umma na Binafsi hapa Nchini

Miradi hiyo ni pamoja na kutengeza Vifaa vya Ujenzi Miundombinu ya Barabara za Tozo na Ujenzi wa maeneo maalum ya Viwanda .

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.