DKT. MWINYI ASHIRIKI MAZISHI YA MAMA WA KAMANDA DAIMA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali katika Maziko ya Bibi Sichana Is-haka Daima Mama Mzazi wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKU) Kanali Makame Abdalla Daima.

Marehemu Sichana Daima Amefariki Jana wakati akitibiwa katika Hospitali ya Mkoa Lumumba. Awali Dkt. Mwinyi alishiriki Sala ya Maiti katika Msikiti wa Bumbwini Misufini. 

ZAIDI YA WATANZANIA 200 WAREJEA KUTOKA DUBAI

Zaidi ya Watanzania 200 waliokuwa wamekwama katika Nchi za Falme za Kiarabu kwa Siku kadhaa kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran wamerejeshwa Nchini kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL kupitia Uwanja wa Ndege wa Dubai hadi Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

 

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA UPENDO NA UADILIFU

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dkt, Hussein Ali

Mwinyi Amewasisitiza Viongozi Wakuu Katika Taasisi Za Umma Kuzingatia Upendo,Uadilifu Na Haki Katika Kuwasimamia Wanaowaongoza Na Utekelezaji Wa Majukumu Yao. 

Akizungumza Katika Kongamano La Tatu La Kiimani Kwa Viongozi Wa Serikali Lililoandaliwa Na Afisi Ya Mufti Mkuu Wa Zanzibar, Ameeleza Kuwa Kongamano Hilo Ni Msingi Wa Kukumbushana Umuhimu Wa Kuzingatia Maadili Katika Utumishi Wa Umma Na Jukwaa Muhimu La Kujifunza Uwiano Wa Kazi Kwa Misingi Ya Kiimani 

ZANZIBAR YAANDIKA HISTORIA IFTAR YA WATU 27,345.

Zanzibar Imeandika Historia Ya Kipekee Baada Ya Kukusanya Watu 27,345 Kwa Iftar Ya Pamoja Ya Kitaifa Iliyofanyika Kwenye Uwanja Wa Amaan Complex Mjini Unguja Tarehe 7 Machi, 2027.

Kwa Mujibu Wa Takwimu Zilizotolewa Na Ofisi Ya Mtakwimu Mkuu Wa Serikali Ya Zanzibar, Katika Iftar Hiyo, Wanaume Waliohudhuria Walikuwa 18, 771 Sawa Na Asilimia 68.6% Na Wanawake Ni 8,574 Sawa Na Asilimia 31.4%.

Hii Ni Mara Ya Kwanza Kwa Zanzibar Kuandaa Tukio La Aina Hii Ambalo Huenda Limevunja Rikodi Ya Dunia.

WAFANYABIASHARA SOKO LA KINYASINI WALIA NA MIUNDOMBINU ISIYO RAFIKI

Wafanyabiashara wa Soko la Kinyasini Wilaya ya Kaskazini 'a' Unguja wamesema kuwa Eneo la Soko ni dogo kwa kufanyia biashara zao na linasababisha msongamano baina ya Wafanyabiashra na Wateja.

 Wakizungumza na Kamera ya Biashara na Uchumi ZBC Wafanyabiashara hao wamesema Soko hilo halikidhi kuchukua Watu wengi hali inayopelekea baadhi ya Wafanyabiashara kupanga bidhaa chini na pembezoni mwa barabara. 

HUDUMA ZA KIBINGWA 20 ZATOLEWA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa mageuzi namafanikio makubwa ya utoaji wa huduma za matibabu ya kibingwa kwa Wananchi. 

Akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Prof. Abel Makubi akiambatana na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar Dķt.Mwinyi amesifia huduma hizo ikiwemo matibabu ya Figo ,Moyo na Ubongo kufanyika hapa Nchini ,hatua aliyopunguzia Serikali na Wananchi gharama za kuwapeleka Wagonjwa Nje ya Nchi.

RAIA 40 WA KONGO WAOKOLEWA BANDARI YA LIKONI PEMBA

Jumla Ya Watu 40 Wanaodaiwa Kuwa Ni Raia Wa Kongo Wameokotwa Katika Bahari Ya Mkoni Baada Ya Kuzama Na Chombo Huku Mmoja Akiwa Tayari Ameshafariki Dunia.

Akizungumzia Tukio Hilo Mkuu Wa Wilaya Ya Mkoani Miza Hassan Faki Ameelezea Tukio Hilo Daktari Dhamana Wilaya Ya Mkoni Amesema Majira Ya Saa Tano Mchana Wamepokea Majeruhi 3

VIONGOZI WAHAMASISHWA KUWASAIDIA WANANCHI

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amewahamasisha Viongozi Kuwasaidia Wananchi Hasa Katika Kipindi Cha Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani Ili Kuweza Kuweka Uwiano Sawa Wa Mahitaji.

Mhe. Hemed Ambae Ni Mwakilishi Wa Jimbo La Kiwani, Ametoa Wito Huo Baada Ya Ugawaji Wa Futari Kwa Wananchi Wa Jimbo Hilo Shehia Ya Kendwa Yenye Nyumba Zaidi Ya 1156 Hafla Iliyofanyika Kwenye Uwanja Wa Mpira Wa Mauwanifutari Kwa Wananchi Wote Hasa Wenye Mahitaji Maalum.

WANAOSAFIRISHA MAGENDO WATAKIWA KUCHUKULIWA HATUA

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mgeni Khatib Yahya ameagiza kuchukuliwa hatua kali za kisheria dhidi ya wale waliohusika kutaka kutorosha Magunia 15 ya Karafuu katika Bandari ya Wambaa Wilaya ya Mkoani

MFUMO MPYA WA KUSAMBAZA DAWA ZA KULEVYA WAGUNDULIWA

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar imewakamata Watuhumiwa Watatu wanaosadikiwa kusambaza na kuuza Dawa za kulevywa kwa kutumia mbinu mpya ambayo ni kuchanganya na Dawa za Binaadamu

Akitoa Taarifa kwa Waandishi wa Habari Ofisini kwake Migombani Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar Kanali Burhani Zubeiri Nassoro amesema bidhaa hizo zenye vifungashio zimekamatwa katika Maduka mabali mbali hapa Zanzibar

Subscribe to news
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.