UJENZI WA SKULI MPYA KUTAONDOA MRUNDIKANO WA WANAFUNZI KATIKA MADARASA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amesema Ujenzi wa Skuli mpya kutaondoa mrundikano wa Wanafunzi katika Madarasa.

Katika shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwenye uwekaji jiwe la msingi Skuli ya Kidichi Wilaya ya Magharibi A, amesema Serikali inakusudia kuondosha uhaba wa Madarasa unaosababisha Wanafunzi kusoma kwa mikupuo miwili.

SERIKALI INA MPANGO WA KUJENGA NYUMBA ZA MADAKTARI KILA WILAYA ILI KURAHISISHA UTENDAJI WAO WA KAZI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ina mpango wa kujenga Nyumba za Madakatari kila Wilaya ili kurahisisha utendaji wao wa kazi.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEJIVUNIA KUFIKIA ASILIMIA 150 YA MALENGO YA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amejivunia kufikia asilimia 150 ya malengo ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa Ujenzi wa Skuli mpya Unguja na Pemba hivyo kuvuka malengo ya ilani ya CCM 2020-2025 iliyoelekeza kujengwa madarasa 1,500 ya Msingi na Sekondari Unguja na Pemba kwa miaka mitano.

VIJANA WAMETAKIWA KUTUMIA VYEMA FURSA ZINAZOJITOKEZA NA KUPANGA MIKAKATI MADHUBUTI ITAYOSAIDIA KUPELEKA MBELE UMOJA NA MAENDELEO YA TAIFA.

Wito huo umetolewa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Kongamano la kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 Mhe Hemed Suleiman Abdallah amesema hatua hiyo itasaidia kufikia malengo waliojiwekea ya kujikomboa Kielimu na kujiepusha na vishawishi kwa kuzingatia mila, silka na utamaduni wa Mzanzibar.

WIZARA YA AFYA INAWATAKA WANANCHI KUIMARISHA USAFI KATIKA MAENEO YAO ILI KUJIKINGA NA MALARIA

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ametakiwa Wananchi kuimarisha usafi katika maeneo yao ili kujikinga na maradhi mbali mbali ikiwemo Malaria.

Ametoa wito alipofanya ziara ya kukagua Majaa yameyoonekana kurundikana kwa uchafu na mazalio mengi ya Mbu katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi amesema kutokana na kuongezeka kwa Maradhi mbali mbali ikiwemo Maradhi ya miripuko, Malaria na kuharisha kitengo cha afya ya mazingira imeona ipo haja ya kufanya ziara hiyo katika maeneo hayo ili kuweza kupata suluhisho ya kuondoa tatizo hilo.

WIZARA YA BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA INAKUSUDIA KUTOA FURSA KWA WAFANYA BIASHARA NA KUZITANGAZA BIDHAA ZAO

Ameyasema hayo katika Ziara ya kuangalia hatua iliyofikia ya ujenzi wa mabanda ya maonyesho huko Fumba, Waziri wa biashara na maendeleo ya viwanda, Mh Omar Said Shaaban amesema  Wizara hiyo imetoa fursa kwa Wafanyabiashara kwa lengo la kuwainua wananchi wake kiuchum ili kuweza kuingiza pato la taifa 

Amesema eneo hilo litakua na maeneo mbali mbali kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali sambamba na Ukumbi wa Kitaifa na Kimataifa kwa ajili ya Mikutano ya wadau tofauti.

SERIKALI INAJIVUNIA UTEKELEZAJI WA MALENGO YAKE YA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO

Ameyasema hayo huko Maziwang'ombe Wilaya ya Michweni Mkoa wa Kaskazini Pemba katika uwekaji wa jiwe la msingi la Skuli ya msingi ya ghorofa ya Maziwang'ombe ikiwa ni Shamra Shamra za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Rais amesema serikali itaendelea kujenga Skuli za ghorofa  katika kila eneo la visiwa ili kuwawekea Wanafunzi mazingira bora ya kusomea pamoja na  kushughulikia changamoto za kimaslahi  kwa Walimu. 

MFUKO WA HIFADHU YA JAMII ZANZIBAR ZSSF UNATARAJIA KUANZA MFUMO MPYA WA UHAKIKI WA WASTAAFU AMBAO UTASIMAMIWA NA MASHEHA KATIKA MAENEO YAO.

Akizungumza katika kazi ya uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa Pencheni zao na mfuko huo katika uhakiki uliofanyika Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mkoa w aMjini Magharibi, Mkuu wa Kitengo cha uhusiano ZSSF Raya Hamdani Khamis amesema mfumo huo mpya utaanza kutumika Mwezi julai mwaka huu ambapo Masheha wameshakabidhiwa Madaftari maalum ambayo yatahifadha taarifa za wastaafu.

Amesema  kiasi ya Wastaafu elfu 13 na mia tano watafanyiwa uhakiki Unguja na Pemba kukiwa na ongezeko la Wastaafu ukilinganishwa na uhakiki uliofanyika mwezi Julai mwaka jana.

SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBIMNU YA UPATIKANAJI WA HUDUMA MBALI MBALI IKIWEMO HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Akifungua Hospitali ya Wilaya ya kati  Mwera Pongwe , Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema kupitia ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, Serikali imejenga Hospitali kumi za wilaya kwa Unguja na Pemba ambazo zina vifaa tiba pamoja na  Gari za kubebea Wagonjwa.

Mh Hemed ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Afya kuhakikisha Wanaisimamia vyema Hosptiali hiyo na Hospitali nyengine  ili kufikia  malengo yaliyokusudiwa na Serikali ya kuwapatia Wananchi huduma bora.   

SERIKALI ITAENDELEA KUVITUMIA VIKOSI VYA IDARA MAALUM ZA SMZ KATIKA UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria utumishi na utawala bora, Mh Haroun ali suleiman, amesema Serikali itaendelea kuvitumia vikosi vya idara maalum za SMZ katika ujenzi wa Miradi ya Maendeleo.

Akifungua Soko la Matunda na Mbogamboga Donge Mtambile, Waziri Haroun amesema Miradi ya Ujenzi iliyosimamiwa na Vikosi hivyo imeonekana kuwa ya kiwango na kuwataka Wananchi kulitunza Soko hilo kwani ni chanzo muhimu cha kuwainua kiuchumi na kuongeza Pato la Serikali.

Subscribe to News
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.