DK. SHEIN AMEITAKA SERIKALI YA ZANZIBAR KUWASOMESHA WAFANYAKAZI WA KADA MBALIMBALI

Dr Shein

Rais Mstahafu wa awamu ya saba wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein ameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwasomesha wafanyakazi wa kada mbalimbali wakiwemo wa afya ili waweze kutoa huduma bora kwa Wananachi.

Ameyasema hayo mbuzini wilaya ya magharib a katika ufunguzi wa Hospitali ya wilaya ikiwa ni shamra shamra ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar.

 Amesema endapo wafanyakazi hao watapatiwa elimu itasaidia kutoa huduma zilizobora zaidi katika Hospitali za Wilaya zilizojengwa pamoja na kuangalia  mambo muhimu yanayohitajika ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya

Aidha  Dk. Shein amewasisitiza Wakuu wa Taasisi kuacha kuwazuia Wafanyakazi kwenda kusoma kwani watakaposoma wataongeza ujuzi kulingana na mabadiliko ya Sayansi na Teknilogia iliyopo.

Waziri wa afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kufungiliwa kwa Hospitali hiyo kutasaidia Wananchi wa Shehia ya Mbuzini na Shehia jirani kupata matibabu tofauti.

Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wizara ya afya Dk Amour Suleiman amesema Hospital hiyo inatoa huduma zote ikiwemo vipimo, upasuaji huduma nyengine na hadi sasa zaidi ya Wagonjwa laki tatu ishirini na tatu elfu  wameanza kutibiwa.  

Hospital ya Wilaya Mbuzini ni miongoni mwa Spitali zilizojengwa kutoa huduma kwa Wananchi ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar ya kusogeza huduma bora za matibabu kwa Wananchi.  .

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.