RAIS SAMIA ATAKA MAMA NA BABA LISHE WAHESHIMIWE

Rais Wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Amemtaka Waziri Wa Tamisemi Prof. Riziki Shemdoe Kutenga Na Kuyaendeleza Maeneo Yaliyo Kwisha Tengwa Kwa Ajili Ya Shughuli Za Mama Na Baba Lishe Nchini Pamoja Na Kuweka Miundombinu Bora Huku Mama Na Baba Lishe Wakitakiwa Kutumia Nishati Safi Ya Kupiki Katika Shughuli Zao.

Pia Rais Dkt Samia Ameitaka Wizara Ya Fedha Kuweka Mazingira Rafiki Ya Kisera Na Kisheria Ili Wafanyabiashara Ndogondogo Wakiwemo Mama Na Baba Lishe Nchini Waweze Kunufaika Na Mikopo Inayotolewa Na Serikali.

SERIKALI YAIMARISHA MAKAAZI YA WAZEE

Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Imejipanga Kuhakikisha Inaweka Mazingira Mazuri Na Wezeshi Kwa Wazee Kwa Kuwajengea Makaazi Mazuri Na Salama Ya Kuishi Ili Kuondokana Na Changamoto Za Makaazi.

Hayo Yameelezwa Na Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Katika Ziara Yake Mkoa Wa Mjini Magharibi Baada Ya Kukagua Mradi Wa Ujenzi Wa Nyumba Za Wazee Welezo.

Amesema Serikali Itaendelea Kuwathamini Na Kuwatunza Wazee Kwa Kuhakikisha Wanapatiwa Mahitaji Yote Muhimu Ikiwemo Kuishi Katika Mazingira Mazuri, Rafiki Na Wezeshi Kulingana Na Uhitaji Wao.

ZANZIBAR YAKABILIWA NA UHABA WA WATAALAMU WA USONJI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema hali ya Usonji kwa Watoto ni changamoto kubwa katika Jamii, hivyo Serikali ina wajibu wa kuhakikisha inaunga mkono jitihada za kuwasaidia Watoto wanaoathirika na hali hiyo.

TAPHATA WAFATILIA UPANUZI WIGO WA AJIRA KWA WATEKNOLOJIA DAWA

Rais wa Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania(TAPHATA) Bw.Thabiti Milandu amesema uongozi wa chama hicho unaendelea kufanya jitihada za dhati na juhudi za makusudi katika kuhakikisha unafuatilia utanuzi na upanuzi wa wigo wa ajira nchini ambapo taaluma hiyo inazalisha watu wengi na uhitaji ni mkubwa.

NYOKA ALIYEKUWA AKIFUGWA AUAWA BAADA YA KULETA TAHARUKI MAVIMBA

Mkaguzi wa Kata ya Milola, Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP) Aloyce Andrew, kwa kushirikiana na wananchi wa kata hiyo, wamefanikiwa kumuua nyoka aliyekuwa akifugwa ambaye alisababisha taharuki kwa wakazi wa eneo la Mavimba, njia panda ya mnadani na wananchi wengine kushindwa kuendelea na shughuli zao kutokana na hofu.

IGP WAMBURA ATANGAZA MABORESHO MAKUBWA VITUO VYA AFYA VYA POLISI

Mkuu wa Jeshi la Polisi amesema vituo tiba vitaendelea kuboreshwa katika eneo la miundombinu, vifaa tiba na  kuwekeza katika raslimali watu ikiwemo kuajiri wataalamu wapya wa Afya.

IGP Wambura ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akifungua mkutano wa Wakuu wa vituo tiba, Wahasibu na Watendaji wa Kikosi cha Afya.

Alisema Jeshi la Polisi linaendelea kuboresha matumizi ya TEHAMA hivyo amewataka kuwa wepesi katika kujifunza na kutumia mifumo iliyopo ili kutoa huduma bora  kwa wateja wa ndani na nje wanaopata huduma katika hospitali za Polisi.

TANESCO LINDI YAPOKEA VITENDEA KAZI VYENYE THAMANI YA BILIONI 1.09 KUBORESHA HUDUMA YA UMEME

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Lindi limepokea vitendea kazi vipya vyenye thamani ya Shilingi bilioni 1.09 kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi.

Vitendea kazi hivyo ni pamoja na Magari madogo mawili , Malori mawili, Bajaji Saba Pikipiki kumi na kompyuta nane

SAFARI FIELD CHALLENGE YAPONGEZWA KWA KUWA CHACHU YA KUKUZA UHIFADHI NA UTALII.

Timu ya Safari Field Challenge imepongezwa kwa mchango wake katika kuongeza ujuzi na ufanisi wa waongoza utalii ambayo ni chachu ya kutangaza utalii na kuimarisha uhifadhi nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya kutembelea timu hiyo katika eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Ndutu, ambapo ameisifu kwa juhudi zake za kuitangaza Tanzania ndani na nje ya mipaka yake.

WANANCHI WAOMBA KASI YA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA IONGEZEKE

Wananchi wa Kijiji cha Kaole Ufundi ,Bagamoyo Mkoani Pwani wameiomba Serikali kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya Dawa za kulevya ili kukomesha biashara hiyo katika Jamii.

Wananchi hao wametoa kauli hiyo wakati Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini DCEA ikikamata virobo 18 vyenye vifurushi 1062 vya dawa za kulevya aina ya Mirungi, Boti ya Mwendokasi pamoja na watuhumiwa Wanne waliokuwa wanasafiri na chombo hicho katika ufukwe wa Magambani Kaole Ufundi, Bagamoyo Mkoa Pwani.

DKT. MWINYI ATEMBELEA MJI WA AFCON FUMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameutembelea mradi wa Mji wa Afcon Fumba uliopo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika Ziara hiyo Dkt. Mwinyi amembatana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Riziki Pembe Juma, pamoja na Wadau wa Mradi wa Afcon Fumba Zanzibar.

Subscribe to news
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.