Lusi Nikolaieva Raia wa Ukraine ameisifu Sekta ya Afya Zanzibar kwa kuwekeza katika huduma ya Mama na Mtoto iliyomsaidia kujifungua salama hapa Zanzibar tofauti na mategemeo yake
Amesema Wanawake wa ndani na nje hawana haja ya kuwa na wasiwasi kwani uwekezaji wa Zanzibar katika Hospital za Serikali ni sawa na Hospital binafsi Bara la Ulaya
Moja ya Watu aliowataja Lusi katika safari yake ya kupata huduma bora ni Muuguzi Maryam na hapa anatueleza hatua hiyo ilivyompa uzoefu na kuongeza maarifa kwa kujisikia fahari katika kazi yake

Lusi anarejea kusema Madaktari wamempa ushirikiano pamoja na kutaja ubora wa vifaa akifafanisha huduma hizo ni sawa na Hospital za binafsi katika Bara la Ulaya
Waliofanikisha kumshawishi Lusi Nikolaieva ni Daktari Hamadi Khalfan nae anatueleza alivyomshawishi na kujenga imani na Madaktari wa Zanzibar
Hata hivyo Daktari Hamad anasema kuna umuhimu wa kuweka chumba binafsi chenye faraja ikiwa ni matamanio ya mioyo yao
Mwisho Lusi anaungana na Mama yake Sara Nikolaieva kuthibitisha uwekezaji katika Sekta ya afya ni wa kupigiwa mfano huku akihimiza Raia wa Kigeni kuzitumia Hospital za Wilaya na kuwa Balozi Duniani

