MIUNDO MBINU BORA YA BARABARA NI CHACHU YA MAENDELEO

CCECC
English

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed amesema lengo la Serikali la kuendelea kujenga miundombinu ya Barabara ni kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa Wananchi na Taifa.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt .Khalid Salum Mohamed akizungumza wakati wa Ziara ya kukagua vifaa vya ujenzi wa Barabara vya Kampuni ya CCECC amesema vifaa hivyo vimekuja wakati sahihi na vitarahisisha ujenzi wa Barabara za Mjini 

 

Akizitaja sababu zilizosababisha kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa Barabara za Mjini Dkt.Khalid amesema  ni pamoja na ujenzi holela unaopelekea gharama za ulipaji wa fidia na kutumia fursa hiyo kuwataka Wananchi kutojenga karibu na hifadhi ya Barabara

Aidha Dkt Khalid ametumia fursa hiyo kuwataka Wananchi kuwa na imani na  Serikali katika ujenzi huo na kuwapongeza CCECC kwa hatua waliofikia na kuwataka kuongeza Watendaji ili kukamilisha Ujenzi wa Barabara hizo 

 

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.