Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesetoa wito kwa Wadau wa Sekta Binafsi kushirikiana Serikali kuekeza katika Miradi ya ubia kati ya Sekta ya umma na Binafsi hapa Nchini
Miradi hiyo ni pamoja na kutengeza Vifaa vya Ujenzi Miundombinu ya Barabara za Tozo na Ujenzi wa maeneo maalum ya Viwanda .
Dkt Samia ameyasema hayo katika ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara Jijini Dar Es Salaam ambapo amesema tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo Mwaka 2021 limeendelea kuwa chomuhimu cha ushauri kwa Seerikali kuhus namna bora ya kuimarisha Biashara Nchini
Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema utakuwa Dira ya kutatua matatizo yanayozikabili shughuli za biashara Nchini na amepongeza Uzinduzi wa Tanzania Digital Economy Strategic Framework, ambayo itafungua ukurasa mpya wa Mapinduzi ya Kidijiti ili kuongeza na kuimarisha fursa za Uchumi.