Habari

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAPANGA MIKAKATI YA MWAKA MPYA WA FEDHA

     Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Fedha na Mipango Dkt.Sada Mkuya Salum amewataka Wafanyakazi wa Wizara hiyo na Taasisi zilizopo chini yake kuhakikisha wanatekeleza mipango kazi iliyopitishwa katika Mkutano Mkuu wa Bodi ya Wafanyakazi.

     Akizungumza na Wafanyakazi hao katika Mkutano wa Mwaka Mpya wa Fedha na Bodi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo Mhe.Sada amesema lengo la Mkutano ni kupanga utekelezaji mpya wa Mwaka wa Fedha ili kutoa huduma bora kwa Wananchi.

SMZ YAJIPANGA KULETA MAGEUZI SEKTA YA KILIMO

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuleta mageuzi ya kilimo nchini kwa kukifanya kilimo biashara chenye tija kwa kuimarisha mnyororo wa thamani kutoka shambani hadi kwa mlaji.

     Dkt.Mwinyi aliyasema hayo tarehe 3 Julai 2024 alipofungua maonesho ya saba ya kilimo ya Nane Nane Zanzibar katika viwanja vya Dole , Kizimbani Mkoa wa Mjini.

WIZARA YA NISHATI NA KIWANDA CHA SUKARI MTIBWA WAJADILI UJENZI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME

    Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema, Wizara ya Nishati na Kiwanda cha sukari cha Mtibwa wapo kwenye majadiliano ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 132 ili kukidhi mahitaji ya Kiwanda cha Mtibwa.

     Mhe. Bashe ameyasema hayo katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kiwanda cha Mtibwa alipokuwa akizindua bwawa la kumwagilia miwa.

DKT.MWINYI ASHUHUDIA UZINDUZI WA USAFIRI SGR

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mke wake Mama Mariam Mwinyi wamehudhuria Uzinduzi wa Usafiri wa Treni ya Umeme kwa kutumia Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) wakitokea Jijini Dar es salaam hadi Dodoma. 

     Mradi huo wa kimkakati umezinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia alianza safari akitokea Dar es salaam kupitia Morogoro na kuwasili Dodoma. 

RAIS SAMIA AZINDUA SAFARI YA TRENI YA SGR KUTOKA DAR ES SALAAM HADI DODOMA

Kiasi cha fedha Shilingi Trilioni 10 zimetumika katika ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR )kwa vipande vya kutoka Dar Es Salaam hadi Dodoma ikiwa dhamira ya Serikali ni kutanua Wigo wa kibiashara ambapo Reli hiyo inatarajiwa  kufika hadi Nchi za Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

WAFANYAKAZI KUMI NA TANO WA ZECO KUSIMAMISHWA KAZI KWA KUIBA UMEME.

Tabia ya Wafanyakazi wa Shirika la Umeme  kujiungia Umeme bila ya  kufuata  utaratibu na Sheria  zilizowekwa kumesababaisha baadhi ya Wafanyakazi wa shirika hilo kusimamishwa kazi kwa kupitisha uchunguzi.

Akizungumza na Wafanyakazi wa Shirika hilo Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe Shaibu Hassan Kaduara amesema  kutokana na kukiuka Sheria na maadili ya kazi Shirika hilo halitomvumilia Mfanyakazi yoyote atakae bainika kuliibia  Shirika ilo.

UJENZI WA BUSTANI YA MWANAMASHUNGI KUKAMILIKA KWA WAKATI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba kuhakikisha Ujenzi wa bustani ya Mwanamashungi unakamilika kwa kipindi Kifupi ili kutoa nafasi kwa Wananchi kulitumia eneo hilo.

SMZ KUENDELEA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA

Wakati huo huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Msarifu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kuajiri Watumishi wapya Elfu Moja na 50 na Ujenzi wa Hospitali 10 za Wilaya Unguja na Pemba, Hospitali ya mkoa, Lumumba yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 208 kwa wakati Mmoja.

RAIS SAMIA AMEIAGIZA WIZARA YA AFYA KUKAMILILISHA UTAFITI WA KITAIFA

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Afya kukamililisha utafiti wa Kitaifa utakaobainisha hali halisi ya Wataalamu wa Afya Nchini waliopo kwenye Soko la Ajira, mahitaji na namna bora itakayoiwezesha serikali kutatua tatizo la kuajiri katika sekta hiyo.

HOSPITAL YA ABDALLA MZEE IMETAKIWA KUNUNUA MTAMBO MPYA WA KUCHOMEA TAKA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba kuhakikisha ndani ya kipindi cha Mwezi Mmoja wamenunua Mtambo mpya wa kuchomea Takataka za Hospitali ili kuepusha madhara.

Akikagua uendeshaji na utoaji wa huduma katika Hospitali hiyo amesema Uongozi unatakiwa kujipanga kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana kwa wakati unaostahiki amesema kuwepo kwa Mtambo huo kutawasaidia Wafanyakazi kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.