Habari

SMZ YAJIPANGA KUIIMARISHA TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR ZBS

     Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza juhudi za kuiimarisha Taasisi ya Viwango Zanzibar ZBS kwa lengo la kuinusuru Zanzibar kuwa Jaa la uingiaji wa Bidhaa hafifu na zisizo na Viwango.

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza katika  Uzinduzi wa Kituo kipya cha Ukaguzi wa Vyombo vya Moto kilicho chini ya ZBS   Maruhubi chenye uwezo wa kukagua Gari Mia Tatu kwa Siku kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa.

DAR ES SALAAM ,TANGA NA MTWARA BEI YA PETROLI YAPANDA 6.3% NA DIZELI 2.2%

     Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Yatangaza Bei Kikomo za Bidhaa za Mafuta kuanza kutumika mwezi Agosti 7, 2024 kwa Mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Mtwara.

     Bei ya Mafuta ya Petroli imepanda kwa bei ya reja reja kwa Dar es Salaam 3231, Tanga 3229, Mtwara 3304.

    Bei ya Dizeli imepanda kwa Dar es Salaam 3131, Tanga 3138 na Mtwara 3140.

      Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 6.3 kwa Mafuta ya Petroli na asilimia 2.2 kwa Mafuta ya Dizeli.

 

DKT.MWIGULU AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA (SADC)

     Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC) unaofanyika kwa njia ya mtandao kwa siku mbili (tarehe 6-7 Agosti, 2024) kutokea Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dares Salaam.

JESHI LA POLISI LATOA MAFUNZO YA UOKOZI WA AJALI ZA KWENYE MAJI

     Katika kuhakikisha ulinzi na Elimu vinatolewa Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Wanamaji nchini kimeendelea kuyafikia makundi mbalimbali yawatumiaji wa vyombo vya majini ambapo leo kimetoa elimu ya ukatili wa kijinsia na mbinu za namna bora za kujiokoa pindi inapotokea ajali katika vyombo hivyo.

WAZIRI MAZRUI AWATAKA WAZAZI KUWANYONYESHA WATOTO ILI KUWAKINGA NA UTAPIAMLO

       Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui ameitaka jamii kulipa mkazo suala la unyonyeshaji wa ziwa la mama pekee katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ili kuwakinga watoto na aina zote za utapiamlo unaojumuisha matatizo ya upungufu wa virutubishi mwilini.

DKT.MWINYI AKUTANA NA MABALOZI WA MAREKANI NA QATAR

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe David Concar aliyemaliza kipindi chake cha miaka minne ya uwakilishi nchini Ikulu Zanzibar aliyefika kumuaga.

     Baadae pia amekutana na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Mhe. Fahad Rashid Al Marekhi tarehe 

NEEMA YAWASHUKIA MAMA LISHE WA SOKO LA KINYASINI

    Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Zanzibar, Abdi Mahmoud Abdi ameliagiza Baraza la Manispaa Kaskazini 'a' kuweka mikakati ya kupunguza Kodi ili kuwapa  unafuu Mama Lishe wa Soko la Kinyasini

    Akizungumza na Mamalishe huko Kinyasini katika Shamrashamra ya Tamasha la Kijana na Kijani litakalofanyika Oktoba 10, amesema Soko hilo limejengwa kwa ajili ya Mamalishe wa Maeneo hayo hivyo kuweka mazingira wezeshi ya Kodi itakayowasaidia kujikwamua na Umasikini.     

TAASISI YA SAZANI TRUST YAONESHA UMUHIMU WA ZIARA ZA KIMASOMO KWA WANAFUNZI

    Ziara za Kimasomo kwa Wanafunzi imetajwa kuwa ni njia mojawapo ya kuwaongezea uelewa kwa baadhi ya mambo ambayo Wanafundishwa Darasani.

SERIKALI KULIPA FIDIA WANANCHI UJENZI WA BARABARA

     Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzu Dkt. Mngereza Mzee  Miraji amesema Serikali italipa Fidia kwa Wananchi ambao wameathiriwa na Ujenzi wa Barabara.

       Akizungumza katika Ziara ya Kukagua  Barabara zinazojengwa katika  Mkoa wa Kaskazini Unguja amewaomba  Wananchi wasiwe na  hofu na Fidia zao.       

DKT.SAMIA ATOA AGIZO UZALISHAJI SUKARI

     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda na Biashara kuangalia namna ya kuweka sera zitakazosaidia uzalishaji wa Sukari ya Viwandani ili kuisaidia Serikali kutoagiza Bidhaa hiyo Nje ya Nchi.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.