Katika kuhakikisha ulinzi na Elimu vinatolewa Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Wanamaji nchini kimeendelea kuyafikia makundi mbalimbali yawatumiaji wa vyombo vya majini ambapo leo kimetoa elimu ya ukatili wa kijinsia na mbinu za namna bora za kujiokoa pindi inapotokea ajali katika vyombo hivyo.
Akitoa elimu hiyo katika Boti ya Kilimanjaro Mkuu wa Dawati la jinsia na Watoto kutoka kikosi cha wanamaji Mkaguzi wa Polisi INSP Avelina Temba amewaomba wananchi hao kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio na maadili katika jamii.
INSP Avelina ameongeza kuwa wazazi wanapaswa kufuatilia kundi la Watoto ambalo tafiti zake zimeonyesha kuwa kundi hilo liko katika hatari ya ukatili ambapo amewataka kuwasikiliza Watoto ili kuzitambua changamoto wanazopitia.
Nae Mkaguzi wa Polisi INSP Anna Ugomba amebainisha kuwa lipo kundi la kina baba ambalo wanapitia katika ukatili ambapo amewataka kutoa taarifa hizo kwa Jeshi la Polisi ili wahusika wa vitendo hivyo wachukuliwe hatua za kisheria.
Sajenti Hassan Mtumwa ambaye ni mzamiaji (Diver) wa kikosi cha wanamaji cha Jeshi la Polisi nchini ametoa Elimu na mbinu za namna bora ya kujiokoa pindi ajali zinapotokeaa katika vyombo vya majini na matumizi sahihi ya viokozi.
Nae Vivienne Maleko mbali na kushukuru Jeshi la Polisi amesema kuwa amekuwa akifatilia kipindi chote ambacho amekuwa Uingeleza amebainisha kuwa amekuwa akifatilia katika vyombo vya Habari namna Jeshi hilo linavyotoa elimu kwa wananchi huku akiwaomba kuendelea kutoa elimu hiyo kujenga uelewa kwa watumiaji wa vyombo hivyo.
Hajal Ismail amesema kuwa elimu hiyo inapaswa kuendelea kutolewa kwa wananchi ili kuwa salama pindi ajali za majini zinapotokea.