Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda na Biashara kuangalia namna ya kuweka sera zitakazosaidia uzalishaji wa Sukari ya Viwandani ili kuisaidia Serikali kutoagiza Bidhaa hiyo Nje ya Nchi.
Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa Agizo hilo wakati akiweka Jiwe la Msingi Kiwanda Kipya cha Sukari cha K4 kilichopo Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro ambacho kinajengwa kwa zaidi ya Shilingi Bilioni 700, ikiwa ni Ziara yake ya Kikazi ya kukagua Miradi mbambali inayotekelezwa na Serikali.
Kutokana na hali hiyo Mawaziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe wamezungumzia namna Kiwanda hicho kitakavyokuwa mkombozi kwa uzalishai wa Sukari Nchini na kuwanufaisha Wakulima.
Awali Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametembelea Chuo Kikuu Mzumbe kisha Kuzindua Mradi wa Ujenzi wa Majengo ya Kampasi Mpya ya Chuo hicho Mkoani hapa na kukipongeza kwa kuendelea kutoa Wataalamu mbalimbali Serikalini.