Habari

UWT YASHAURI KUONGEZWA ADHABU KALI MAKOSA YA UBAKAJI NA ULAWITI

     Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amepanga kushawishi kutungwa  sheria kali itakayowabana wanaopatikana na makosa ya Ubakaji na Ulawiti.

     Chatanda ametoa kauli hiyo huko  Ukerewe wakati akihutubia Mikutano ya hadhara kwa nyakati tofauti katika Vijiji vya Kagunguli, Nansole na Mjini Nansio.

    Amesema kuongezeka kwa vitendo hivyo kunalazimisha kuwepo kwa sheria ambazo zitadhibiti vitendo hivyo viovu.

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA UJASIRIAMALI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

    Wananchi wametakiwa kutumia fursa za ujasiriamali zinazopatikana katika Maeno yao ili kujikwamua Kiuchumi kwa shughuli wanazozifanya. 

    Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh.Zuberi Ali Maulid amesema hayo katika Uzinduzi wa Soko la Wajasiriamali Wananwake Fujoni lilojengwa kwa Mfuko wa Maendleo wa Muwakilishi wa Jimbo Bumbwini.

    Amesema Wananchi wanatakiwa kuthamini juhudi  za Viongozi za kuwaletea maendeleo  na kuwakwamua  na umasikini Mh.Zuberi amewashauri kuitunza Miundombinu ya Soko hilo ili idumu kwa Muda Mrefu.

TAMASHA LA KIZIMKAZI DAY KUZINDULIWA TAREHE 18 MWEZI HUU

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuzindua Tamasha la Kizimkazi  Kizimkazi Day Tarehe 18 Mwezi huu.

     Akitangaza Wadhamini wa Tamasha hilo Mwenyekiti wa Tamasha Mahfoudh Said Omar, huko Hoteli ya  Kwaza Kizimkazi amesema Maandalizi ya Tamasha hilo yanaendelea vizuri  ambapo Mwaka huu litakuwa bora zaidi  kuliko Matamasha yote yaliopita.

DKT.MWINYI AWAONGOZA WANANCHI MAZIKO YA MZEE WALID FIKIRINI

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaongoza Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi mbalimbali katika Maziko ya Mzee Walid Fikirini Aliefariki na Kuzikwa Kijijini kwao Kikombe-Tele Mkoa wa Kaskazini Unguja.

     Marehemu Walid Fikirini wakati wa uhai aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa  Kamisheni ya Utalii pamoja na kuhudumu nafasi mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU MKOANI RUVUMA WAJITOKEZA KUCHANGIA DAMU

    Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Ruvuma chini ya Taasisi ya 'JAI' Tanzania wamejitokeza kuchangia damu safi na salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya taasisi hiyo kitaifa ambapo ufanya shughuli mbalimbali za kijamii.

      Mratibu wa Huduma Salama Mkoa wa Ruvuma Fredrick kihaule amewashukuru wachangiaji damu wote waliojitokeza kuchangia damu kwani wamegusa kwa kiwango kikubwa sana cha mahitaji ya damu katika hospitali ya Mkoa.

RAIS DKT.MWINYI AZINDUA KAMPENI YA KIJANA KIJANI ''TUNAZIMA ZOTE TUNAWASHA KIJANI ''

    Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amewahakishia Vijana kuwa Serikali imekusudia fungu la fedha ili kuwawezesha katika Elimu , Ajira na Uwezeshaji.

    Rais Mwinyi aliyasema hayo katika Uwanja wa New Complex Amaan wakati wa alipozindua kampeni ya kijana kijani ya Tunazima zote Tunawasha kijani iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi .

MAKAMO MWENYEKITI WA CCM AMEWATAKA WANACHAMA KUTOYUMBISHWA NA MANENO YA WAPINZANI.

Makamo Mwenyekiti wa CCM ZAnzibar Dkt, Hussein Ali Mwinyi amewanasihi Wanachama wa CCM kutoyumbishwa na maneno ya Wapinzani na badala yake kuwa kitu kimoja ili kuleta ushindi wa Chama hicho.

Ametoa tamko hilo wakati akizungumza na Wajumbe wa kamati za Siasa ngazi mbali mbali za Mkoa wa mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema Ubaguzi ni jambo baya na amekemea kutorudia katika siasa zinazoashiria Uvunjifu wa Amani, chuki na vurugu za kisiasa.

TEKNOLOJIA YA KILIMO KUMELETA MABADILIKO SEKTA YA KILIMO NA UFUGAJI.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman amesema kukuwa kwa matumizi ya teknolojia ya Kilimo nchini kumeleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Kilimo na UFugaji.

Amesema hayo wakati alipotembelea Maonesho ya Wakulima ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Dole kizimbani Wilaya ya Magharibi “A”. 

Amesema Maonesho yanatoa fursa kwa Wananchi kupata Taaluma ya kuweza kulima na kufuga kwa kutumia Mbinu za kisasa ambazo Mkulima huweza  kuvuna Mazao mengi kwa muda Mfupi.

RAIS DKT.MWINYI ASEMA DENI LA ZANZIBAR BADO NI HIMILIVU

    Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inakusanya shilingi bilioni 300 kila mwaka kwa kulipa madeni na Serikali inaweza kulipa deni lolote na bado ni himilivu.

    Dkt.Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 8 Agosti 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake alipozungumza na Kamati za Siasa za Matawi, Wadi , na Majimbo za Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ukumbi wa CCM Mkoa.

JUMUIYA YA WAHITIMU WALIOMALIZA MASOMO CHINA (OZACA) YAZINDULIWA

     Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar imesema itaendelea  kuimarisha ushirikiano  na Serikali ya China ili kuchochea Maendeleo katika Sekta ya Uchumi, Elimu na Utamaduni.

    Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe.Shaaban Ali Othman wakati Akizindua Jumuiya ya Wazanzibar Waliosoma China OZACA  huko kwenye  Ukumbi wa Ofisi ya Ubalozi Mdogo wa China Mazizini 

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.