Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman amesema kukuwa kwa matumizi ya teknolojia ya Kilimo nchini kumeleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Kilimo na UFugaji.
Amesema hayo wakati alipotembelea Maonesho ya Wakulima ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Dole kizimbani Wilaya ya Magharibi “A”.
Amesema Maonesho yanatoa fursa kwa Wananchi kupata Taaluma ya kuweza kulima na kufuga kwa kutumia Mbinu za kisasa ambazo Mkulima huweza kuvuna Mazao mengi kwa muda Mfupi.
Mhe. Hemed amesema Serikali itaendelea kuimarisha eneo la Maonesho ya Wakulima ili liweze kutoa huduma bora kwa Wakulima . Waziri wa Kilimo, maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis amesema mwamko wa Wafanyabiashara katika maonesho hayo umekuwa Mkubwa na kuvuka lengo la kusajili Wajasiri Amali 500
Nao Washiriki wa maonesho ya Nane Nane nafaidika na huduma na kupatiwa Elimu juu ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa wenye tija zaidi.