SERIKALI KULIPA FIDIA WANANCHI UJENZI WA BARABARA

KATIBU MKUU ZIARA

     Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzu Dkt. Mngereza Mzee  Miraji amesema Serikali italipa Fidia kwa Wananchi ambao wameathiriwa na Ujenzi wa Barabara.

       Akizungumza katika Ziara ya Kukagua  Barabara zinazojengwa katika  Mkoa wa Kaskazini Unguja amewaomba  Wananchi wasiwe na  hofu na Fidia zao.       

    Nao baadhi ya Wananchi katika Ziara hiyo wameiomba Serikali  kuzingatia mambo muhimu wakati wa Ujenzi wa  Barabara ili kupunguza athari zinazojitokeza mara kwa mara.

     Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Barabara Zanzibar Mhandisi Cosmas Masolwa amewashauri Masheha kusaidia kusimamia hifadhi za miundombinu ya  Barabara ili  ziendele kudumu kwa Muda Mrefu.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.