DKT.MWIGULU AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA (SADC)

DKT.MWIGULU NCHEMBA

     Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC) unaofanyika kwa njia ya mtandao kwa siku mbili (tarehe 6-7 Agosti, 2024) kutokea Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dares Salaam.

     Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (Mb), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Saada Kassim Msemo, na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali wanashiriki mkutano huo.

    Mkutano huo unajadili masuala ya utangamano wa Jumuiya hiyo, ikiwemo hali ya kiuchumi katika nchi wanachama pamoja na kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo wa Kikanda wa SADC utakaotumika kutatua changamoto mbalimbali za upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango na miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo.

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.